UCL
Member
- Aug 18, 2020
- 8
- 6
Vuguvugu la Uchaguzi linazidi kupanda kila tunapoikaribia siku ya October 28. Ni siku inayosubiriwa na watanzania walio wengi ili kutimiza haki yao ya Kikatiba
Kimsingi Uchaguzi ni mchakato unaoambatana na tofauti miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu. Si tu kila chama kina imani ya kushida bali pia mgombea na wafuasi wake wana tumaini kubwa la kuibuka kidedea. Mwamuzi wa kati (Central referee) katika mpambano huu ni Tume ya Uchaguzi. Ni dhahiri HEKIMA watakayoitumia katika maamuzi hususan katika kipindi hiki, itatufanya kuiona ng'ambo ya pili kwa AMANI pasipokuwa na makovu ya mioyo
Mbali na kwamba nao ni binadamu wanaoweza kujaribiwa, kushawishiwa ama kuwa na maslahi hali kadhalika mapenzi binafsi, wanatakiwa kumshirikisha Mungu aliye hai katika utekelezaji wa majukumu yao uwanjani. Waifanye kazi yao kwa kumpendeza Mungu na si kumfurahisha mwanadamu. Tunamwomba Mungu kamwe asiruhusu roho ya uzembe na upendeleo kutawala mioyo ya watumishi hawa bali haki na mapenzi mema kwa Taifa letu vikatamalaki kila hatua wanayoipiga katika kipindi hiki.
TANZANIA BILA MACHAFUKO YA KISIASA INAWEZEKANA. AMANI NA IWE KWENU.