NEC kugawa upya majimbo ya uchaguzi

NEC kugawa upya majimbo ya uchaguzi

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Posted by: Sarafina Lidwino 3 hours ago

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imepanga kuyagawa upya majimbo ya uchaguzi nchini. Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema, tume yake tayari imekamilisha ugawaji majimbo hayo na muda wowote itaanza mchakato wa kuyagawa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jaji Lubuva amesema, tume yake imeamua kugawa majimbo hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikana wa mawasiliano, hali ya kijiografia na alichoita, "kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2010."

Aidha, Jaji Lubuva amesema, Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia uwepo wa miundo mbinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo moja na jingine, simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakae harakisha maendeleo katika eneo husika.

NEC inatangaza majimbo mapya ya uchaguzi, huku uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapigakura, ukiwa umedolola.

Amedai kuwa kuna baadhi ya majimbo ni makubwa kulinganisha na majimbo mengine, jambo ambalo linatokana na ongezeko la watu nchini.

"…zoezi hili linatakiwa kufanyika mara kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10. Ugawaji wa majimbo ulifanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na kwa kuwa sasa tunaelekea katika uchaguzi mwingine, lazma tufanye hivyo," ameeleza Jaji Lubuva.

Amesema utaratibu utakaotumika katika ugawaji wa majimbo hayo na kubadilisha mipaka, ni kuwasilisha maombi ya kufanya hivyo, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, kwenda kwa katibu tawala, katibu tawala za mikoa, kisha kwenda NEC.

Hata hivyo, mara baada ya kuwasilishwa maelezo hayo, baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani wadai kuwa ugawaji huo wa majimbo unafanyika kwa shinikizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Tume imezidiwa na majukumu; wanataka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, huku muda ukiwa haupo," alisema Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF).

Alihoji, "walikuwa wapi siku zote, wakati muda uliobaki hautoshi?"

MwanaHALISI Online lilipomuuliza, Dk. Emmanuel Makaidi, mwenyekiti wa chama cha National League Democrat (NLD) amesema, "NEC inafanya kazi za CCM."

Akiongea kwa uchungu, Dk. Makaidi amesema, "Hii ni tume inapangiwa kazi na serikali, siyo kujipangia. Ni tume mbovu kuliko ile ya Jaji Luis Makame."
 
Yaani ccm wanadhani kuongeza majimbo ndo kutawaokoa kweli..? Yaani wanaleta siasa kwenye mambo ya msingi.. Wanataka kuongeza majimbo ili wabunge wafikie 1000..? Na kwa akili zao zilivyokuwa ndogo wanadhani kwa kuongeza majimbo ndo itakuwa salama kwao punguani hawa..

Na huyu Mzee Lubuva tunamheshimu lakini naona ameamua kujitoa ufahamu.. Hajamaliza moja kubwa anarukia kwenye jingine kubwa zaid..! Anakubali kutumika mzee mzima na heshima zake..!
 
Mkuu achana na kuheshimu punguani hawa, ni shida kwa taifa teknolojia imekuwa badala ya kuunganisha majimbo unayagawa ili kuongeza matumizi ile hali vifaa tiba hakuna???
 
Hali ya hewa ni mbaya sana kwa Ccm na mtagawa hadi nchi October hiyooo kitaeleweka tu
 
Hivi hawa ccm wana akili kweli?
Ss unagawa kwa hela ipi ?
 
Bado naitamani ile rasimu ya Katiba ya Warioba! Ililiona hilo na kulisemea, la idadi kubwa ua wabunge!
 
Yaani huyu mzee lubuvumba ni majanga vibaya sana
 
Nimemkumbuka Jaji Warioba na ile ktaika ya wananchi!
 
Lahaula...!
Unagawa majimbo huku hujui hata idadi ya wapiga kura!
Unagawa majimbo miezi minne kabla ya upigaji kura!
Only in Tanzania!
 
Hii ndiyo mbinu ya kuahirisha uchaguzi iliyokuwa ikisikika kichini chini. Watasema wanasogeza mbele uchaguzi hadi watakappotangza tena ili kwanza wagawe majimbo!. Huu ni wenda wazimu!
 
Lahaula...!
Unagawa majimbo huku hujui hata idadi ya wapiga kura!
Unagawa majimbo miezi minne kabla ya upigaji kura!
Only in Tanzania!

Kuongeza majimbo ni kuongeza gharama. Hii NEC hata hela ya BVR hawajapewa zote serikali kwa nini itumie fedha kwa mambo yasiyo ya lazima? Kwa teknolojia ya sasa ya habari majimbo yanatakiwa yapunguzwe. Lkn ccm ikiongeza tukiingia ikulu kitu cha kwanza ni kuifuta hii tume na kurekebisha katiba na kuunda tume guru.
 
Hii ndo nafuu ya Mwakyembe anaenda kugombea jimbo jipya sijui litaitwaje?
kuanzia Bwato kuelekea Matema.
 
Kuongeza majimbo ni kuongeza gharama. Hii NEC hata hela ya BVR hawajapewa zote serikali kwa nini itumie fedha kwa mambo yasiyo ya lazima? Kwa teknolojia ya sasa ya habari majimbo yanatakiwa yapunguzwe. Lkn ccm ikiongeza tukiingia ikulu kitu cha kwanza ni kuifuta hii tume na kurekebisha katiba na kuunda tume guru.

wewe utakua na nafasi gani kufanya hayo
 
Back
Top Bottom