NEC kuanza mchakato wa kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
lubuuu.JPG

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti ya Uchaguzi kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adam Nyando, amesema kuwa maandalizi ya mchakato huo yanaanza kwa kufanyia maboresho makubwa sheria ya kura ya maoni.

Afisa huyo amesema kuwa kikubwa kwa sasa kinachofanywa na tume hiyo ni kuendelea kutoa elimu kwa mpiga kura ili kumpa ufahamu mwananchi juu ya kutambua haki yake ya kupiga kura.

Tume hiyo ya Taifa inaendelea na zoezi hilo la kukabidhi ripoti ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu iliomalizika Octoba 25 mwaka jana kwa mikoa mbalimbali hapa nchini na jana ilikabidhi katika mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro amesema uchaguzi katika mkoa wake ulienda vizuri isipokua changamoto mbalimbali zilijitokeza ikiwemo usafirishaji wa masanduku kutokana eneo la Delta.

Chanzo: EATV[/SIZE]

Kwa Maoni yangu:
Naishauri serikali iangalie upya namna ya kuipitia rasimu hii ya katiba mpya kwa kuwashirikisha wadau muhimu kwani kwa kiasi kikubwa, bunge la katiba liliendeshwa kibabe na bila uwepo wa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) na vipengele muhimu kuondolewa.

Hii ni kuhakikisha maoni ya wananchi yanazingatiwa na kutuwezesha kupata katiba bora.
 
Hakuna hata sababu ya kutoa elimu kwa mpiga kura

Je ZNZ hawana elimu ya mpiga kura kiasi cha kufuta matokeo
 
My Take kama Mtanzania niliye na uchungu wa maisha haya ya hatunywi supu hatunywi chai...kama ifuatavyo;
1. KUACHA KUTUMIA KODI ZETU VIBAYA KUKABIDHI RIPOTI KWA KILA MKOA SIJUI HATA INA TIJA GANI MAANA KILA MTU ANAELEWA VEMA UCHAGUZI ULIVYO KWENDA.

2. RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA NDIYO TUANZIE HAPO NA SI VINGENEVYO KWA KUFUATA MAONI YA WANANCHI NA SIYO YA KIKUNDI FULANI KWA MANUFAA YAO KWA KUHOFIA DHAMBI ZAO.

TUNACHOTAKA NI RASIMU YA WARIOBA IBORESHWE KWA KUONGEZA VIPENGELE VYENYE MENO HASA KWA WANAOJIITA WATAWALA.
 
Magufuli akiweza kuifanyia kazi rasmu ya mzee Sinde Warioba atakuwa ametengeneza Tz mpya itakayodumu hadi miaka 100 ijayo bila kubadili wala kuongelea katiba tena labda marekebisho madogomadogo tu, na hapo ndo itakuwa rahisi sana kuwa na Tz ya viwanda na hivyo kuifanya nchi yetu iingie kwenye zenye uchumi wa kati zikiongozwa na China, Brazil, Urusi na S. Africa (Nigeria?).

Lakini endapo na yeye ataendeleza mahaba kwa chama na ile katiba yao chini ya 6,bado itakuwa ni vigumu mno kwa tz kupiga hatua mbele maana pindi Magufili aachapo urais hatujui ni aina gani ya atakayefuata. na hivyo kajitihaga alikokaonyesha katakuja liwa ndani ya miezi miwili tu kisha kuanza yaleyale.
 
Nashauri hili la kupigia kura katiba mpya na mchakato wa katiba mpya uhairishwe na wala Magufuli asihangaike nao ....ni jambo lililotupotezea muda na rasilimali kwa manufaa ya wanasiasa uchwara na vigeugeu....

Rais ajikite kwenye yale aliyoyaahidi tu aachane na huu ulaji wa wanasiasa
 
Rasimu inatamka kwamba "ili mtu awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge anatakiwa ajue kusoma na kuandika" wakati sera ya elimu (basic education) inamtaka kila mtoto wa Tanzania afikie elimu ya kidato cha nne ambayo ni ya lazima.
 
Kirerenya,ukawa walisusa mchakato ukapita
Kilichobakia ni ukawa kuwashawishi wananchi wapige kura ya hapana,maigizo kwa sasa hayasaidii
 
Hivi ikatokea kwa mfano inapigiwa kura ya maoni katiba pendekezwa ya mh Sita halafu ukawa wakafanikiwa kuwashawishi wananchi waikatae na kweli wakafanikiwa je,serikali ya ccm itajiuzuru?

Maana David Cameron ameshindwa kule UK na sasa anajiuzuru,nauliza tu....
 
Hawa watu mbona hawana huruma, bado tu wanataka waendelee kuteketeza pesa zetu?
Watuhurumie kidogo basi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
My Take kama Mtanzania niliye na uchungu wa maisha haya ya hatunywi supu hatunywi chai...kama ifuatavyo;
1. KUACHA KUTUMIA KODI ZETU VIBAYA KUKABIDHI RIPOTI KWA KILA MKOA SIJUI HATA INA TIJA GANI MAANA KILA MTU ANAELEWA VEMA UCHAGUZI ULIVYO KWENDA.
2. RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA NDIYO TUANZIE HAPO NA SI VINGENEVYO KWA KUFUATA MAONI YA WANANCHI NA SIYO YA KIKUNDI FULANI KWA MANUFAA YAO KWA KUHOFIA DHAMBI ZAO.
TUNACHOTAKA NI RASIMU YA WARIOBA IBORESHWE KWA KUONGEZA VIPENGELE VYENYE MENO HASA KWA WANAOJIITA WATAWALA.
Kanisa kabisa tuanze na Ratiba ya Warioba, Period!
 
Back
Top Bottom