NEC kuanza mchakato wa kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya

Lubuva nilikuwa namheshimu sana lkn alivyoboronga kwenye uchaguzi mkuu anastahili hukumu ya maisha gerezani
acha ujinga na ulofa wewe. una ushahidi utuwekee hapa wa shutuma zako. au kwa sababu ulishindwa kwenye uchaguzi ndio unamtupia lawama Lubuva.

kwa nini usiwalaumu wananchi ambao waliamua kuchagua wenyewe kwa utashi wao. usitutie hasira saizi. unadhani nani angekupa kura wakati huekeweki. unaita watu mafisadi, baadae unasema sio ulikosea. wakati ulisema una ushahidi wa kutisha na kutosha.

mmekaribisha watuhumiwa wa ufisadi mkasababisha viongozi mahili kama Dr Slaa wakatimka. tena kwa vipesa uchwara tu vya kununuliwa labda. ajenda ya ufisadi mkaizika kifo cha mende. mkasema tu shut up kama hatuna ushahidi wa shutuma zozote. maushahidi yetu yote tukayachoma moto.

hivi wewe ni binadamu wa kawaida kweli kuandika maneno haya? tafakari! !
 
lubuuu.JPG

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti ya Uchaguzi kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adam Nyando, amesema kuwa maandalizi ya mchakato huo yanaanza kwa kufanyia maboresho makubwa sheria ya kura ya maoni.

Afisa huyo amesema kuwa kikubwa kwa sasa kinachofanywa na tume hiyo ni kuendelea kutoa elimu kwa mpiga kura ili kumpa ufahamu mwananchi juu ya kutambua haki yake ya kupiga kura.

Tume hiyo ya Taifa inaendelea na zoezi hilo la kukabidhi ripoti ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu iliomalizika Octoba 25 mwaka jana kwa mikoa mbalimbali hapa nchini na jana ilikabidhi katika mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro amesema uchaguzi katika mkoa wake ulienda vizuri isipokua changamoto mbalimbali zilijitokeza ikiwemo usafirishaji wa masanduku kutokana eneo la Delta.

Chanzo: EATV

Kwa Maoni yangu: Naishauri serikali iangalie upya namna ya kuipitia rasimu hii ya katiba mpya kwa kuwashirikisha wadau muhimu kwani kwa kiasi kikubwa, bunge la katiba liliendeshwa kibabe na bila uwepo wa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) na vipengele muhimu kuondolewa.

Hii ni kuhakikisha maoni ya wananchi yanazingatiwa na kutuwezesha kupata katiba bora.
siyo serikali hii ya kibabe iliyoziba masikio
 
Amesha sema anawalinda watangulizi wake kama katiba iliyopo inavyo walinda, sasa kuna haja tena hapo na katiba ya walioba inayopendekeza washitakiwe?

Hakuna matumaini ya katiba mpya hapa.
 
acha ujinga na ulofa wewe. una ushahidi utuwekee hapa wa shutuma zako. au kwa sababu ulishindwa kwenye uchaguzi ndio unamtupia lawama Lubuva. kwa nini usiwalaumu wananchi ambao waliamua kuchagua wenyewe kwa utashi wao. usitutie hasira saizi. unadhani nani angekupa kura wakati huekeweki. unaita watu mafisadi, baadae unasema sio ulikosea. wakati ulisema una ushahidi wa kutisha na kutosha. mmekaribisha watuhumiwa wa ufisadi mkasababisha viongozi mahili kama Dr Slaa wakatimka. tena kwa vipesa uchwara tu vya kununuliwa labda. ajenda ya ufisadi mkaizika kifo cha mende. mkasema tu shut up kama hatuna ushahidi wa shutuma zozote. maushahidi yetu yote tukayachoma moto. hivi wewe ni binadamu wa kawaida kweli kuandika maneno haya? tafakari! !
POVU
 
Hivi ikatokea kwa mfano inapigiwa kura ya maoni katiba pendekezwa ya mh Sita halafu ukawa wakafanikiwa kuwashawishi wananchi waikatae na kweli wakafanikiwa je,serikali ya ccm itajiuzuru? Maana David Cameron ameshindwa kule UK na sasa anajiuzuru,nauliza tu....
kumbe unawaza tu

ngoja mie nianze kuota iwe hivyo

kwa #Tz hii ya Kusadikika haitokuja kutokea
 
Magufuli atengeneze Rasmu ya Warioba? Labda sio Magufuli huyu tuliye naye
Rasimu ya Warioba. Makonda na Polepole ndani ya Dar es Salaam, katika nafasi TOFAUTI na wakati wa UGUUGU la katiba "Mpya"! Time is the BEST Referee in the life of a person!
 
Yaani kukabidhi ripoti wanaenda mkoa kwa mkoa, huu nao ni ufisadi, mchakato uanzie kwenye rasimu ya warioba

Hata mm nashangaa yaani MKOA KWA MKOA kukabidhi report ya matokeo ya uchaguzi, hii hatari sasa.. jamani jamani.

Mh. Rais Magufuli hili zuia mara moja.. hii tabia gani NEC wanafanya eeeh.
 
Ile rasmu ya mzee warioba kwanini wenye mamlaka hawaipendi sana?
Kwa sababu inawapunguzia mamlaka na kumwongezea mwananchi mamlaka. Watu wanaopenda kutawala badala ya kuongoza hawawezi kuipenda rasimu ya Warioba. Huo ndo ukweli mchungu hata kama inawezekana Jaji warioba mwenyewe keshaitosa rasimu yake!
 
acha ujinga na ulofa wewe. una ushahidi utuwekee hapa wa shutuma zako. au kwa sababu ulishindwa kwenye uchaguzi ndio unamtupia lawama Lubuva. kwa nini usiwalaumu wananchi ambao waliamua kuchagua wenyewe kwa utashi wao. usitutie hasira saizi. unadhani nani angekupa kura wakati huekeweki. unaita watu mafisadi, baadae unasema sio ulikosea. wakati ulisema una ushahidi wa kutisha na kutosha. mmekaribisha watuhumiwa wa ufisadi mkasababisha viongozi mahili kama Dr Slaa wakatimka. tena kwa vipesa uchwara tu vya kununuliwa labda. ajenda ya ufisadi mkaizika kifo cha mende. mkasema tu shut up kama hatuna ushahidi wa shutuma zozote. maushahidi yetu yote tukayachoma moto. hivi wewe ni binadamu wa kawaida kweli kuandika maneno haya? tafakari! !
Hueleweki

Rudia kuandika kama MTU mwenye akili timamu sio hivi umeandika kitahira tahira nitakujibu
 
Mwenyekiti kamaliza za 2015? Mie nadhani mchakato ungeanza upya Mwenyekiti wa tume badala ya warioba awe Polepole DC ili aubebe ccm
 
Hivi ikatokea kwa mfano inapigiwa kura ya maoni katiba pendekezwa ya mh Sita halafu ukawa wakafanikiwa kuwashawishi wananchi waikatae na kweli wakafanikiwa je,serikali ya ccm itajiuzuru? Maana David Cameron ameshindwa kule UK na sasa anajiuzuru,nauliza tu....
Tangu lini matokeo ya namna hiyo yakapitishwa? Umesahau ya Zanzibar?
 
Hivi ikatokea kwa mfano inapigiwa kura ya maoni katiba pendekezwa ya mh Sita halafu ukawa wakafanikiwa kuwashawishi wananchi waikatae na kweli wakafanikiwa je,serikali ya ccm itajiuzuru? Maana David Cameron ameshindwa kule UK na sasa anajiuzuru,nauliza tu....
Utamaduni wa kujiuzulu hat Tz labda mpaka mwaka 2115!
 
Itakuwa ni uhuni na dharau kubwa kwa walipa kodi na Watanzani wengi nchini kama Serikali hii itaamua kutumia mabilioni ya shilingi kupitisha katiba ambayo haikupendekezwa na Watanzania.

Na kama wakifanya hivyo migogoro ya uchaguzi nchini kamwe haitakwisha na inaweza kuwa chanzo cha kuingiza nchi kwenye vurumai kubwa siku za usoni.
 
Back
Top Bottom