VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
kwa UMRI alionao Jaji Lubuva hastahili
kuendelea na utumishi wa Umma tena.
Sijui kwa nini tunang'ang'ania lazima kiongozi wa NEC awe jaji mstaafu. Nafasi hii siyo ya kutoa hukumu au kuitafasiri sheria ni nafasi ya kuongoza taasisi. Tuiache iwe huru kuongozwa na mtu mwenye uwezo, hali na nguvu za kuwajibika.kwa UMRI alionao Jaji Lubuva hastahili
kuendelea na utumishi wa Umma tena.
Hakuna siri tena.Kila kitu kinaonekana. Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC iko taabani.Taabani kiutendaji.Hadi sasa kuna sintofahamu kuhusu mustakabali wa Kura ya Maoni. Haiko wazi kama itafanyika au la.Yote hayo ni kwasababu ya NEC.NEC inajikongoja, tena kwa kutambaa,katika kuandikisha wapigakura. Ndiyo kwanza uandikishwaji kwa njia ya mashine za BVR umefanyika kwa majaribio Kawe na kuzinduliwa Njombe.
Hakukuwa na dalili zozote za kufanikisha uandikishaji huo. Huku Kura ya Maoni ikipangwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu, na kampeni za kuipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ikiendelea, NEC haioneshi dalili za kuendana na muda huo. Leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro ametangaza kugawa rasmi nakala za Katiba Inayopendekezwa. Serikali imetangulia mbele na NEC imebaki nyuma.
NEC inapaswa pia kutoa elimu ya uraia kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muda nao ndiyo unazidi kuyoyoma. Kimahesabu, NEC inapaswa kumaliza uandikishaji na uhakiki wa wapigakura hadi kufikia mwisho wa mwezi huu. Ili, utakapoanza mwezi Aprili elimu ya uraia ianze kutolewa. Kama hiyo haitoshi, NEC ndio watakaosimamia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hakuna dalili zozote za kuanza matayarisho ya zoezi hilo linalobeba mustakabali wa Tanzania yetu kwa miaka mitano ijayo.
NEC ya Jaji Lubuva imechoka.Iko hoi.Kama yabidi,ifumuliwe na kuundwa upya. Bunge litakaloanza kesho liweke hoja ya dharura mezani kuhusu NEC na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kabla mambo hayajaharibika. NEC isaidiwe kwa kurekebishwa. Ama sivyo,madhara ya kimaumivu ya kisiasa kwa kila mwanademokrasia hayatavutia. Wabunge,kazi ni kwenu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kweli kabisa mkuu, kuna siku niliwahi kuweka uzi hapa kuhusu Mzee Lubuva kuwa amechoka kimwili na kiakili hawezi hii kazi, na haoni hatari ya mbeleni kwa taifa hili endapo mambo yatavurugika kwa watu kukosa haki yao ya msingi. Ifike mahali mwenyekiti wa tume ya uchaguzi si lazima awe jaji anaweza kuwa mtu yeyote mwenye uwezo. Kenya walikuwa na kijana mdogo kabisa Bw. Isack kama sikosei alikuwa around 40yrs. Sasa leo tunakuwa na mtu hata kumbu kumbu zimeanza kumtoka bado tunampa majukumu mazito na yenye kugusa maslahi mapanda na mustakabali wa nchi yetu.
Taifa hili watu 45 milioni kweli tunakosa mtu makini atufanyie hii kazi??????
Kigogo chama chetu mahiri kimechoka, kimezeeka, kimeishiwa kila aina ya mipango mkakati. Sasa hakijielewi, nimesikitishwa na mpango mkakati wa Kinana na Nape Nnauye kutembea na fisi, ili kuvuta watu mikutanoni, wanataka kujustify nini... Najua wana uhakina na maddudu toka katika vyombo vya kiserikali kusaidiwa ikiwezekana mabavu.JK ndio wa kulaumiwa..angalia wenzetu Kenya wanaongozwa na vijana kwenye tume ya uchaguzi..sisi tunachukui hii mizee iko kwenye menopause ndo tunaipa mamlaka ..haya sasa bvr vurigu tupu mpaka tunaenda kuazima Kenya ! Aibu
Umenena mkuu, mambo ya kutumia mabavu hayatafanikiwa. Maridhiano ya hatua kwa hatua na wadau wote ni muhimu katika jambo hili. Kuweka kura ya maoni Aprili 30 ni moja ya mfano hai wa kutaka kutumia mabavu, mambo mengine hayaendi hivyo.
Ila huenda pia ni mgomo baridi maana ya kura ya maoni ilipaswa kutangazwa na tume, lakini mkuu wa kaya akajichukulia majukumu ya kutangaza.
Halafu NEC wana kauli nyingi kweli kweli
Mzee Tupatupa