NEC CCM kukutana Dodoma Nov 21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC CCM kukutana Dodoma Nov 21

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 15, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tuesday, September 15, 2011, 13:28

  Rai-Makala  • Kutoka wamoja au maneno ya Nyerere kutimia
  • Taarifa ya hali ya siasa nchini kuwasilishwa
  • Gamba, makundi, Igunga kujadiliwa
  Na Mwandishi Wetu
  KIKAO cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakachofanyika mjini Dodoma Novemba 21 na 22, mwaka huu kinatarajia kutoa majibu juu ya masuala mbali mbali ambayo yamechangia vurugu, kurushiana maneno makali na kuhujumiana ndani ya chama hicho .


  Kikao hicho kitakachofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, pamoja na mambo mengine kitapokea taarifa ya hali ya kisiasa itakayosomwa na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Siasa, January Makamba.


  Tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CCM haijatulia. Makundi ambayo Mwenyekiti Rais Kikwete aliomba yavunjwe, ndio kwanza yameongeza mpasuko. Hivi sasa kuna mpasuko wa kundi la Wanamtandao, mpasuko uliosababishwa na kura za maoni katika uchaguzi wa 2010.


  Lakini hoja kubwa zaidi ambayo NEC ya CCM lazima itoe jibu ni hili la kuhujumiana. Sio siri tena kwamba kuna watu ambao wamepania kwamba lazima wamrithi Rais Kikwete 2015 na ndicho chanzo kikuu cha chokochoko.

  Mambo mengine yatakayowekwa mezani ni pamoja na uchaguzi mdogo wa Igunga, uchaguzi ambao wachambuzi wanasema umeonyesha dhahiri kwamba CCM hamkani si shwari tena kwakuwa ilipata ushindi mwembamba licha ya kutumia nguvu kubwa na fedha nyingi.


  Pia anatarajiwa kuzungumzia siasa za CCM na CHADEMA mkoani Arusha, siasa ambazo kwa kiasi kikubwa zimevuruga hali ya amani na utulivu katika mji huo wa kitalii nchini.


  Mkutano huo muhimu unafanyika baada ya wenyeviti na makatibu wa mikoa wa CCM kuitwa Dar es Salaam wiki iliyopita, ambapo pamoja na mambo mengine walipendekeza viongozi wawili wa chama hicho Samuel Sitta na Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wachukuliwe hatua kwa kukihujumu chama hicho kwa makusudi.


  Viongozi hao wanatuhumiwa kutoa kauli na misimamo ambayo ni yao binafsi, lakini wamekuwa wakiwahadaa Watanzania kuwa ni msimamo wa CCM, na kwamba ina baraka za chama.


  Dhana ya kujivua gamba ambayo iliasisiwa na Rais Kikwete mjini Dodoma Februari 5, mwaka huu, pia inatarajiwa kutawala sehemu kubwa ya mjadala huo, hasa baada ya kupotoshwa na Nape na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Chiligati, mjini Dodoma walipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao cha NEC mwezi Februari.


  Vyanzo vya habari ndani ya CCM vimesema kuwa, lengo la dhana hiyo kukipa sura mpya chama hicho, ili kiendane na wakati pamoja na kukidhi mahitaji ya wapiga kura ambao wengi ni vijana.


  Lakini baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho wanatuhumiwa kubadili mantiki na dhana nzima ya kujivua gamba, kwa kuanza kuwaandama watesi wao wa kisiasa, kiasi cha kupendekeza wafukuzwe kwenye uanachama.

  Kutokana na upotoshwaji huo, siasa za makundi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekidhoofisha chama hicho, sasa zimeshika kasi na kuibua makundi mawili, wale wanaojiita wasafi na wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Katika kikao hicho, pia mgogoro uliopo ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) unatarajiwa kujadiliwa, lengo likiwa kurejesha hali ya amani utulivu ndani ya chombo hicho muhimu kwa uhai wa chama hicho.


  Hali mbaya ya uchumi, kuporomoka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa bei za vyakula, tatizo sugu la ajira miongoni mwa vijana, ni miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujadiliwa.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kali kweli nani atabaki CCM? Vizee au Vijana?
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Kama kweli Nape ameugua kama ilivyoripotiwa humu, nashiwishika kuamini kuwa ugonjwa wake unahusiana na kikao hiki. Msongo wa mawazo au vinginevyo.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna watakaoenguliwa umo!
   
 5. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dokezo la Kwanza: Taarifa inawasilishwa na Mkuu wa Idara Ya Mambo ya Nje na siyo Katibu Uenezi na Itikadi wala siyo Katibu Mkuu.

  Dokezo la Pili: Watu watatu wametajwa majina kwa kukipotosha chama, ila mmoja wao katajwa mara mbili.

  Dokezo la Tatu: Katibu Uenezi na Itikadi hadi wiki hii hakuwa amepewa dondoo za mkutano huu (sina hakika kama sasa anazo au la), wakati Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Makamba na wajumbe wengine wawili wamekuwa wanatayarisha taarifa hizi kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

  Dokezo la Nne: Mkutano wa Wenyeviti na Makatibu wa mikoa ulifanyika wakati Katibu Uenezi na Itikadi 'katumwa' Marekani 'kusuluhisha mgogoro' wa tawi. Kipi muhimu kati ya tawi jipya la ughaibuni au mkutano wa wenyeviti/makatibu?

  Hayo madokezo manne yatakupa picha nini kinaendelea au kinapikwa.
   
 6. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nitafurahi wakitoka makundi makundi na makando vinywani mwao kama watakavoingia.
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  tatizo lao huwa wanatumia masaburi kwa kila kitu. kufikiri, kunena na kunaniiii............mwishowe wanatoka na maagizo ambayo wenyewe ndo wanaotakiwa kuyatekeleza. CCM ni kama ch....a aliyekwisha soko
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Na mimi nimeliona hilo..wameanza kuwaweka sawa ki saikolojia wajumbe ili haya yaanze ku-sink into their minds and hearts...Kambi ya akina Nape ikiwa na majeruhi wengi na pia ikiwa imepewa karipio kali kwa atakaye thubutu kuendelea na kuwanyooshea vidole 'watwana'...Aise mimi naona utabiri wangu karibu kutokea ...Thanks Jesus for truly you are my lord and saviour
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  That power is with u..just send a word of confusion to the camp of the enemy....Malaika wako tayari kulibeba hilo neno mpaka hapo na kuwa tawanya kama vile mnara wa babel...Hakuna ushirika wa wachawi unaodumu...

  In Jesus name I decree in one door they will enter and unto seven shall flee from that meeting. All traps set for the innocents let catch those very ones who set them...Every curse directed to the righteous back to the sender and any arrow thrown to the anointed one let it go back to the sender with seven times more speed.....Let all men know these that in Jesus there is glory and by these let all creation bow unto him and each tongue confess that He is Lord of Lords..
   
Loading...