Ndumba

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
26may14-thats-just-odd.jpg
 
ndumba na ngae hii tumuulize mtu mmoja anaitwa kwa jina mganga wa kienyeji aje hapa atuambie hii ndio kitu gani mkuu mbuzi mzee.

Ndugu yangu mzizimkavu, kiukweli tiba zetu zinatofautiana kutokana na maeneo. Na tiba zinabadilika kulingana na aina ya ugonjwa na mgonjwa. Ziko tiba zinatumia elimu ya vitabu vya tiba na nyengine zinatumia Mizimu. Kwa hiyo zile za elimu ya vitabu hazitofautiana sana kwa sababu ni kama stand hivi, lakini za Mizimu hubadilika na ziko ambazo hujawahi hatakuziona au kuzisikia. Inategemea na huo mzimu ulio kuja kutoa tiba utakavyo taka na kufanya. Lakini pia kuna Waongo na Matapeli kwenye fani kama zilivyo fani nyengine. Kwa hiyo tahadhari ni muhimu kuchukuliwa hasa unapokua na tatizo ambalo linahitaji attention yetu.

Kwa mfano, kinacho onekana kina endelea hapo, kiganga tunaweza kukuita chano. Yaani sadaka au chakula maalum kwa mizimu, ili kumfanya mgonjwa apate nafuu au kuwaita mizimu waje wasaidiane na sisi katika matatizo yanayo mkabili binadamu mwenzetu. Kimsingi hiyo tiba inayofanyika hapo ipo kimizimu zaidi. Kinacho onekana hapo ni mikate na matango. Vile vile waganga wanaokana wame vaa nguo za kike, hivyo mizimu inatarajiwa kuhudhuriwa hapo ni Mzimu ya kike. Ndio maana waganga wame vaa sidiria na sketi.

ESENTE
 
Asante kwa kutujuza Mkuu MGANGA WA KIENYEJI hapo mgonjwa ninaona anatambikwa ili matatizo yake yaishe aweze kupona asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo staili ya bembea ni ya aina yake. Hivyo vitu mdomoni ni matango kweli? Mbona vinaonekana kama nyeti za kiume! Mikate kwa sausage za matango.
 
Back
Top Bottom