Ndugu zetu mlioaminiwa na Rais chondechonde

WAZIWAZI

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
1,815
1,575
Tunawaomba sana ndugu zetu mlioaminiwa na Rais wetu JPM akawapa nafasi mbalimbali kumsaidia kuongoza nchi hii mjtahidi kuwa wazalendo kwa kumshauli na kumwambia uhalisia wa mambo yanayoendelea katika taifa hili ili atimize azima yake nzuri ya kutukomboa.

Tumeona mazuri mengi tu kama kununua ndege ili tupate watalii wengi na kuingiza fedha za kigeni kwa ajili ya kutekeleza miladi mbalimbali hapa nchini, tuliona alivyochukua hatua za haraka kuikwamua MUHIMBILI suala la vitanda, madawati ya wadogo zetu, kufuta kodi za mazao kama korosho na hatimaye kafuta kodi kwenye kahawa hayo ni baadhi ya mambo ambayo mtu mwenye akili timamu lazima ampongeze.

Kuna dalili zinaonekana huenda mkuu anapokea taarifa zisizo sahihi sana kutoka kwa watu anaowaamini; ni mawazo yangu tu huenda siko sahihi, ila tunawaomba ndugu zetu mliopewa madaraka na Rais wetu mlitendee haki taifa letu kwa kusema na kushauli ukweli daima.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 
njia rahisi ni kufanya kama mafuru, nenda kwa vyombo vya habari ongea point zako, hata akikutumbua tutakua tumesha jua sababu ya kutumbuliwa kwako. asije akaleta sababu nyingine kama za boss wa tanesco
 
Back
Top Bottom