Ndugu zangu, mbona tunaiendea Point of No Return?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Watanzania wenzangu sasa itoshe!!

Je si vizuri sasa tukaweka kando ushabiki wa kivyama ili kwamba fahamu zetu zirejee, na kuweza kuyaona mambo katika usahihi wake?
Na ni hapo tutakapozingatia jambo hilo ndipo tutaanza kujihoji maswali ya msingi juu mustakabari wa huu mkondo tata wa kisiasa uliotukumba na kututeremsha kwa kasi bondeni mithiri ya upepo wa kisurisuri.

Kwa nini nasema hivi?

Nachelea hivi isije ikawa kumbe ndiyo polepole lakini kwa hakika, kama taifa; kisiasa, tukawa tunazielekeza nyayo zetu kuindea point of no re'turn!

Awiiiiiii, jamani, nalia kwa uchungu! chonde chonde wandugu kukingali na mapema hebu tusiruhusu kamwe nyayo za taifa hili kusimama mahali hapo pa kutisha!
Na kwa vyovyote vile, iwe ni kwa wema au kwa ubinafsi, katika kudumisha umoja na mshikamano wa taifa letu, sote tungejihadhari sana ili tusijekumfanya mmoja wetu au kikundi cha watu kuigusa point hiyo!

Hivyo ni wajibu wa kila mmoja miongoni mwa wadau wa kisiasa kutengeneza au tuseme kupalilia ridhiko la kweli ndani ya moyo wa mwenzake, bila kujali ni upande wa utawala au wa upinzani.

Kamwe usiwepo upande unaopeleka maumivu au kero kwa mwenzake, huku upande huo kwa makusudi mazima ukipuuzia kelele zinazotokana na maumivu hayo!
Kuendelea kufanya hivyo ni kuwafanya watu waifikie point hiyo mbaya hata kama walikuwa hawataki kufika huko.

Ni rahisi mno kwa yeyote yule aliyejaaliwa utashi kujifanya hamnazo juu ya hiki ninachokielezea sasa, lakini hata hivyo baadaye; hilo halitamfanya asalimike dhidi ya ukweli huu uliosimama wima mithiri ya dira ambayo huelekea kaskazini daima.
Hii ni kwa sababu natambua vipaji vya ubishi walivyonavyo wengi wetu humu, ila ni vema pia wakaelewa kuwa; ukweli hubaki kuwa ukweli, mpaka uje wakati mkweli, utakaoufunua ukweli huo peupe!

Ndugu kamwe tusiombe kukutana na viumbe au kiumbe aliyefika mahari ambapo hawezi kurudi katika meza ya mazungumzo.
Mtu huyu kando na kutothamini maisha ya wengine lakini pia huwa hathamini maisha yake!
Huyu ni mtu ambaye huwa hajali utu tena ingawa ana mwonekano wa kibinadamu!
Hapo huwa ni unyama juu ya uhayawani tu!

Aghalabu katika historia; ambaye kwa hakika ni mwalimu mzuri, hakuna mtu au watu waliowahi kujifikisha wenyewe kwenye point of no re'turn.
Wengi wao walifikishwa na jamii zao wenyewe kulingana na misukumo ya kimaslahi iliyokuwepo wakati huo.

Katika hili bado tuna mengi ya kujifunza pindi tunapoyatazama mataifa yanayosimama mahari hapa ambapo ni pagumu pa kurejea kutoka katika ukatiri wa kibinadamu uliopindukia!
Tazama Iraq, Afughanstarn, Siria, Libya, DRC, Somaria, Burundi, nk.
Je tuna chochote cha kujifunza kutoka katika njia zilizowafikisha katika point waliyoifikia?

Je wao hawakuanza hivi tulivyoanza sisi leo?
Je mamlaka zetu hazina upuuziaji ambao mamlaka zao zilikuwa nao?

Ndugu zangu ni rahisi kama nini kwa mtu mwema kujifunza uovu kuliko mtu mwovu kujifunza wema.
Katika taifa hili ili tuendelee kudumisha amani hii iliyopo nawashauri watawala watengeneze utaratibu utakaosimamia haki kwa kila mtu, kwa kila chama, kwa kila taasisi iwe ndogo au kubwa.
Yaani kila mtu na kila kitu kiwe sawa mbele ya sheria ili haki itendeke, na ionekane na wote kutendeka.

Hii hali ya sheria kuonekana kumbana huyu na kumwachia yule, kamwe, narudia tena kamwe, haitatuacha salama siku zote!
Hii hali ya chama hiki kuzuiwa kufanya siasa na kile kuwa huru kuendelea, kamwe haitatuacha salama.
Haya na mengine ya aina hiyo yakiendelea kushabikiwa na wasiojua madhara yake; baadaye yatakuja kugunduliwa kuwa ndiyo zilikuwa hatua za kuelekea katika point of no re'turn.

Wakati umewadia ambapo kila mtu anapaswa kuwa mkweli na kuacha unafki wa kisiasa unaoweza kuligharimu taifa hili na kupelekea msambaratiko wake!

Mungu ibariki Tanzania ya mabibi na mababu zangu.
 
Kuna tatizo kwani wakati amri ni kuishi kama shetani? Hakuna namna kaamua iwe hivyo na ndivyo inavyo ellekea kuwa.
 
Nilishasema..kuna baadhi ya watanzania wamerukia 'band-wagon' ya upinzani bila kujua inawapeleka bondeni...wajanja walisharuka nje toka 2015!
 
Back
Top Bottom