Ndugu yangu Dkt Mwakyembe madaraka yana nini?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Juzi juzi ulitoa tamko kuhusu vyeti vya ndoa, Mh Rais akatengua, likaja suala la Ney wa Mitego ambako nina uhakika kua ulihusika kwa kiasi kikubwa juu ya kukamtwa kwake na kuufungia wimbo wake lakini pia Mh Rais akatengua.


Kwakweli madaraka yana utamu wa aina yake, yaani mtu maamuzi yako yanatenguliwa mara mbili mfululizo bado unaendelea na kazi tu. Kwa sifa ya mwanasiasa wa kweli wala asingeendelea kuaibika kiasi kile. Mtu ukishaona maamuzi yako yanatenguliwa mara kwa mara kajitafakari,inawezekana haufai kwa nafasi yeyote ile.
 
Ndugu tatizo katiba ni mbovu sana, yani hata sheria iwe nzuri vipi mbele ya hii katiba utoki.... Rais kama mungu
 
Kwa Mwakyembe naona hilo sio tatizo..

Muhimu kwake ni madaraka..

Hawa ndio type ya wale viongozi ambao wakipigwa chini huwa wanalia wiki nzima.
 
Anasema acha alipwe fadhila maana yeye ni mamrehemu sasa kwa ile sumu aliyopewaga! Ni kama fadhila asije akasema ukweli bure ikaja kuwa shida!!
 
Back
Top Bottom