Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,644
Nachukulia mfano kwangu kwanini nampenda sana mama. Naamini bila baba nisingezaliwa ama kupata elimu kidogo niliyonayo lakini ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa mama amechangia sana kunilea na kujifunza maisha na hivyo kutokea kupendwa sehemu yoyote ninayoenda kuishi hata na marafiki zangu pamoja na mke wangu hata siku naoa siku hiyo hiyo kama mama alivyoniambia kuwa nimpatie masharti yangu mke siku ya kwanza ya kumweka ndani kwa sauti tulivu ili asije kuzoea ndipo umwambie taratibu zako kwani atakuona ushamchoka na sasa unaanza kuandaa misuguano. Nilimwambia kama kuna watu wa kuheshimu ikiwezekana hata kwenda chuo cha heshima basi ni baba na mama yangu.
Tukiwa zaidi ya watoto 10 mimi nimeshuhudia wadogo zangu wakizaliwa kulelewa lakini ni mama aliyekuwa hapati usingizi mara ananiamsha kwenda kuchimba dawa usiku kwa tatizo la michago ya utotoni huku baba akiwa hayuko serious ama kuguswa na hali ya mgojwa kama mama. (Baba na mama wanapendana na hadi leo wako pamoja kijijini).
Nimejifunza mambo mengi sana kwa mama na bila kuficha mama zetu ukiwafuatilia wako tayari hata kutoa uhai wake kwa ajili ya mtoto wake (wale wanaotupa watoto naamini wanafanya hivyo wakiwa katika msongo mkubwa wa mawazo aidha kwa kutelekezwa na wanaume na anajikuta kwao amefukuzwa na hana msaada wowote.
Nina mengi sana ya kumsemea mama lakini tajaza server bure. Tukio lililonifanya nimkumbuke mama tena ni lile tukio la Beslan Rusia katika shule ya watoto wadogo mwaka 2004 pale magaidi wa Chechniya walipoiteka shule hiyo kubwa siku ya kufunguliwa kwa mhula mpya ambapo wazazi hushiriki na kuwa na watu zaidi ya 1000.
Mama mmoja akiwa na watoto watatu alipewa option ya kuondoka na mtoto wake mchanga na kuwaacha wale wawili lakini akakataa na kuuwawa pamoja na watoto wake huku yule mchanga akimpatia mtu ambaye alikubaliwa na magaidi kuingia na kufanya nao negotion ambazo hata hivyo zilifeli baada ya Putin kukataa kuiachia Chechniya mikononi mwa waasi wenye itikadi kali. Much respect to Pagi my mama.
Hivyo basi popote nilipo, lolote nifanyalo huwa nakumbuka mama kwanza japo hata baba sina ugomvi naye, ninafanana naye sana hadi shangazi siku moja ashawahi kunipa heshima ambayo hutolewa tu kwa kaka mtu (salamu ya kisukuma) akifikili mimi ndiye kaka yake (baba).