Ndugai apinga watumishi kuishia kusimamishwa tu, ataka wafukuzwe!

Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,450
35,177
Dodoma.Spika Job Ndugai ametaka operesheni ya kushughulikia wazembe kazini iongezwe nguvu kwa kuunda sheria ya kuwatimua badala ya kuwasimamisha kazi kwa uchunguzi kama inavyofanyika sasa.

Ndugai, ambaye ni kiongozi wa Bunge ambalo kazi yake ni kutunga sheria, alimuomba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumshauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupeleka haraka bungeni muswada wa sheria itakayoruhusu watumishi wazembe wafukuzwe badala ya kusimamishwa kazi.

Kauli ya Ndugai imekuja wakati Taifa likiwa kwenye mjadala kuhusu vitendo vinavyofanywa na viongozi wa Serikali vya kusimamisha watu kazi kwa kutangaza tuhuma zao kwenye mikutano ya hadhara na baadaye kuagiza uchunguzi ufanyike jambo ambalo wadau wa utawala bora na wanaharakati wanasema ni ukiukwaji wa sheria.

Wadau hao wanasema watuhumiwa hawana budi kuchunguzwa kwanza kabla ya kutangazwa hadharani kuwa wana makosa, wakisema kutofanya hivyo ni kushawishi uchunguzi ufanyike kwa lengo la kuwatia hatiani badala ya kutafuta ukweli.

Akizungumza kwenye kikao cha Makamu wa Rais na viongozi wa CCM mkoani Dodoma jana, Ndugai alisema sheria iliyotungwa ya watumishi wa umma si nzuri kwa kuwa inatumika kuwalinda hata wasiostahili kuwapo kazini kutokana na uzembe na ubadhirifu.

“Sheria za kuwalinda watumishi hazifai, ni bora mkamshauri AG azilete zote bungeni kwa wakati mmoja tuzipitishe ili wazembe na wabadhirifu wafukuzwe si kusimamishwa,” alisema Ndugai.

Alisema wakati mwingine amekuwa akishangaa kuona jinsi watu wanavyoharibu, lakini wakitaka kufukuzwa sheria inakuwa kikwazo na kulifanya Taifa kuingia katika hasara.

Alisema sheria hizo zikipelekwa bungeni atazisimamia zipitishwe haraka zote kwa wakati mmoja ili kuondokana na dharau inayofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa na huruma na taifa lao.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa alikiri kuwa nafasi ya chama katika ngazi ya chini ni ndogo kwani CCM inaonekana kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa pekee.

Kimbisa aliwataka madiwani na watumishi wengine kutomwangusha Rais na badala yake waache kuwanyenyekea watumishi wa Serikali, bali wawawajibishe pale inapobidi.

Chanzo: Mwananchi
 
Safi sana Ndugai, alafu tunasubiri na ile sheria ulioisema itungwe ya kuondoa kipengele cha permanent and pensionable kwenye ajira za serikali maana kinaleta uzembe kwa wafanyakazi
 
Asante sana spika, kweli una UCHUNGU na nchi yako!! Shida ni wale waliotaka MABADILIKO ya KUZUNGUSHA MIKONO.

Kuna watu uchaguzi 2020 WANAWEZA wakapigwa mawe watakaposema WANATETEA WANYONGE!!!
Queen Esther
 
Safi sana Ndugai, alafu tunasubiri na ile sheria ulioisema itungwe ya kuondoa kipengele cha permanent and pensionable kwenye ajira za serikali maana kinaleta uzembe kwa wafanyakazi
Uchunguzi muhimu then ndo MTU atajwe hadharani. Hiyo ije haraka sana maana kuna watu wanafanya ajira zao peke yao. Halafu wanajisahau sana
 
Asante sana spika, kweli una UCHUNGU na nchi yako!! Shida ni wale waliotaka MABADILIKO ya KUZUNGUSHA MIKONO.

Kuna watu uchaguzi 2020 WANAWEZA wakapigwa mawe watakaposema WANATETEA WANYONGE!!!
Queen Esther
Haya mambo yafanyike kweli tuone vitendo tu.
 
Nice insights Mkuu Spika.

Tanzania inahitaji sana fikra kama hizo ili iweze kusonga mbele.

-Kaveli-
 
Cha ajabu wabunge hawa hawa akiwemo Ndugai walifuta kipengele cha wabunge wasio na tija kuwajibishwa na wapiga kura wao kama kamati ya Warioba ailivyopendekeza, lakini kwa watendaji anataka express dismissal. Kwangu huu ni UNAFIKI sheria ziwabane wote kwa uwiano.
 
Ndugai jichunge sana, tunajua fika kuwa mwenye mamlaka kwa sasa ni NS Dr Tulia hivyo matamko yako lazima update kibali chake la sivyo anaweza kukuchapa memo bure.
Kumbuka alivyo amua kurudisha serikalini mabilioni ya shs nawe kusoma maamuzi nayo whatsupp
 
Ha ha ha du, lkn mbona watumish Wa umma vipi kuhusu wanasiasa
 
hongera Ndungai.
Maana benchi limejaa watu wengi waliotumbuliwa huku wakifaidi mishara bila kazi,
Nchi hii iwe na option mbili tu uadilifu au uwezi wapishe wenzako
 
Ndugai yuko sahihi, sheria hizi zipitiwe upya, Mfano Tume ya maadili ya viongozi wa umma wakati Chenge anaitwa kuhojiwa na Tume kumbe kuna sheria inayozuia asihojiwe (vigogo) angalia watumishi ngazi za chini sheria ni mara moja inafanya kazi, kesi ni nyingi huko idara za kazi, yaani hizi sheria ni butu kwa wakubwa na zimeletwa na wasomi wa nchi hii..
 
Wafanyakaz wa serkali safar hii hawana chao, kila anayesimama anaona wao ndo wakuongelea na kufukuzwa nadhani hii imewafundisha outcome za kujipendekeza, so uchaguzi wa 2020 sababu wao ndo wanasimamia, watajitahid kuwa fair.
 
Cha ajabu wabunge hawa hawa akiwemo Ndugai walifuta kipengele cha wabunge wasio na tija kuwajibishwa na wapiga kura wao kama kamati ya Warioba ailivyopendekeza, lakini kwa watendaji anataka express dismissal. Kwangu huu ni UNAFIKI sheria ziwabane wote kwa uwiano.
daah jamaaa unaona mbali saana, kudos, eti ndugai naye mzalendo , hahaaaa
 
Ndugai yuko sahihi, sheria hizi zipitiwe upya, Mfano Tume ya maadili ya viongozi wa umma wakati Chenge anaitwa kuhojiwa na Tume kumbe kuna sheria inayozuia asihojiwe (vigogo) angalia watumishi ngazi za chini sheria ni mara moja inafanya kazi, kesi ni nyingi huko idara za kazi, yaani hizi sheria ni butu kwa wakubwa na zimeletwa na wasomi wa nchi hii..
yy( ndugai) mbona alipiga mtu wakati wa mchakato wa uchaguzi, hakuchukuliwa hatua yoyote
 
Back
Top Bottom