Ndoto yangu

Ndoto yangu

TAECOLTD

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
1,051
Reaction score
1,845
Bila shaka hili si neno geni masikioni mwako, kwanini unashauriwa kuwa na ndoto? Umewahi kujiuliza hiyo ndoto ni ya aina gani na ina manufaa gani kwako?

Vijana wengi hawafanikiwi au niseme asilimia kubwa ya watu wanaoishi kwenye nchi masikini hawafanikiwi sababu kuu ikiwa "hawajui haswa ndoto wanayoitaka ni ya aina gani" ujue kuna aina nyingi ya ndoto na baadhi ni ndoto zenye ujumbe malum hizi huziita za ki-Mungu, ndoto za mateso hizi huziita za kishetani ingawa kwangu siamini na ndoto za abunuasi yaaan ndoto zilizopo ndotoni yaaan haziwezekani

Ndio sio kila ndoto inawezekana kwako acha kujidanganya na kujifariji, wake up ulimwengu uliopo ni reality na sio fantasy world so wake up.

Watu wengi sana hupenda kusoma makala za maendeleo na kujiunga magroup mengi ya ushauri kama WhatsApp, Facebook na mengineyo mengi tu ila miaka nenda miaka rudi wapo pale pale wakisugua benchi na msemo wao "one day yes" hakuna siku itayofika ila siku ni leo na sasa hivi start from scratch

Wengi wanapenda sana kupanga malengo ila [emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42] hayatimii wanahisi ni uchawi, no my friend hamna uchawi ila uchawi ni wewe. Hujali muda, hujali pesa hata ikiwa mia just imagine hiyo mia unayoidharau unajua mia mia hiyo kila siku kwa mwaka ni 36,600 je hiyo ni hela ndogo? Nikupe mfano anuai kabisa bila kupepesa maneno kuna wakati nilipigika nikaumiza kichwa nikaamua kuongea na wuza baa kadhaa niwe nawapelekea sigara wanauza then tunapigiana hesabu na kulipana. Nilipata baa kama nne za kuuza sigara na trust me per day nilikua nalaza mpaka 12 faida ilikua miaka mingi kabla Mungu hajafungua milango yake ila baadae hizi baa zilifungwa moja baada ya nyingine na nyingine sababu ya bomoa bomoa ya jiji so biashara ile ikafa.

Mwanazuoni Lewis Carroll amewahi nukuliwa akisema "kama hujui unapokwenda basi njia yoyote itakupeleka" yaaan kuwa na ndoto ni jambo moja ila kua na mpango kazi ni jambo lingine

Ni sawa na ile kauli ya kwamba "kulea mimba si kazi bali kazi kulea mwana", so ndugu kua na lindoto likuuuuubwa lisilokua na strategic plans is a total wastage of your time. Anza na ndoto ndogo then iwekee malengo na mpango kazi uitimize then enenda ukiset malengo yako utajishangaa miaka kadhaa upo umbali ambao hutaamini ila huu mfumo wa kuendelea kujifariji na maneno ya kutia moyo sijui utafanikiwa na blah blah zingine utajishangaa miaka kumi bado upo katika groups mbali mbali unasoma articles za kutia moyo na namna ya kufanikiwa

Nikutakie mfungo mwema na ijumaa njema ndugu
 
"Ndoto si kuzikalia, skani mkilialia.
Ndoto nikuamka, mbio kuzikimbilia..."

Alisikika Joh Makini akitamka maneno hayo.
 
Back
Top Bottom