harakat
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 2,887
- 1,350
Maisha ya binadamu yanahitaji maono , maono ambayo watu wengine huyaita ndoto kuzifikia ndoto hizi huitaji kufanya kazi Kubwa kuzielekea.
Naam kutimiza ndoto ni maajaliwa ya mwenyezi Mungu nami ndoto yangu ya kuwa Rais Wa hii Nchi ikitimu nitajitahidi sana kufanya Yale ya msingi kuhakikisha makundi yote kwenye jamii yetu yananufaika na rasilimali za Nchi yao bila kujali wana toka maeneo gani hii itasaidia kupunguza na kuondoa ukanda .Nimeona kila linalifanyika watu huzungumza na unapokua Rais kumbe unakua Rais Wa wananchi wako wewe ni MTU Wa kila MTU hivyo watu wako wanayo haki ya kukuzungumzia wewe kama taasisi yao ya kwanza ktk Nchi husika .Hapa kumbe nitapaswa kuwavumilia wale wanaonikosoa na wale wanaonisifia niwaangalie kwa makini isijekua wananing'ong'a .Kukosolewa kunakuwa ni kawaida tu lazima watu wakokosoe maana wewe ni wakwao ukikosea wamekosea na madhara watayapata kwa kiasi kikubwa tu hivyo hili linakua ni la kuangalia kwa maana Yake.
Pia nitajitahidi kuangalia kwa makini timu nitakayokua nayo mfano mawaziri ,wakuu Wa mikoa na taasisi za serikali lazima wawe watu watakaoleta tija kwa taifa watu watakaochochea ukuaji Wa uchumi na watakaoendana kabisa na muktadha Wa vision yangu ya wakati huo.
Mfano kama itakua ni ishu ya kuboresha Elimu na miundombinu basi lazima nitahakikisha kila kitu kama ni vyeti vinafanyiwa ukaguzi Mimi nitaanza na vya kwangu na kufuatiwa na wale Wa karibu yangu . Hii ni ili kuhakikisha heshima ya Nchi pamoja na kuishi yale ninayoyaamini na kuyasimamia yanakuwa yanafanyika kwa ukamilifu bila kuacha chembe ya ubabaishaji na mashaka.
Ndoto yangu hii ni ya msingi sana maana ni ndoto ambayo inahitajika umakini Wa hali ya juu kuifikia .Fikiria wananchi wanatakiwa wakuamini na kukukabidhi Nchi hivyo lazima uwe muadilifu katika kutenda na kusema ili kuisogelea ndoto hiyo.
Nikiifikia nitajitahidi pia kuhakikisha nachanganya haina zote za uongozi pale inapohitajika.
Kuna Udikteta huu utatumika pale ambapo mambo yatakua hayaendi na kila nikiangalia ninayo sababu ya msingi ya kupenyeza nguvu zangu za kikatibakufanikisha mambo ya kimsingi katika Nchi yangu.
Demokrasia hili aina pia itapewa nafasi yake kwa mapana maana ukuaji Wa Demokrasia utasisimua pia ukuaji Wa uchumi na maendeleo ya jamii husika pia itafanya watu wengi zaidi kujihusisha na kujiona wapo na wanashirikishwa kwenye maamuzi na hivyo kuelewa nafasi zao na kujituma ipasavyo.
Katika hili kuna kipindi nitakua kama mfalme pia hili litasababisha hawa wengine wachukua majukumu yao na kutenda kama inavyotakiwa maana muda wote ukiwafuatilia hawataonekana kama wanafanya kazi hata kidogo .Wafalme huwa wanasikiliza na kutatua tatizo wakiwaachia viongozi Wa kisiasa kufanya shughuli muhimu zinazowahusu pia kama Rais nitatulia kuwapa nafasi na kuangalia wanayoyafanya kama wako na vision yetu au la ,pia nitajitahidi kuhakikisha ushirikishwaji Wa hali ya juu kutoka kwa wananchi wangu unapatikana .
Naamini kuna kipindi serikali itashikilia kila kitu kama italazimika kufanya hivyo ili kuokoa maslahi ya Nchi .Suala la maisha ya wananchi kuboreshwa litapewa kipaumbele cha hali ya juu mno maana wananchi ndio watakua mabosi wangu sio kwamba Mimi nitakua juu ya sheria hapana nitajitahidi mno kuhakikisha serikali inatenda kama inavyotakiwa.
Utawala Wa kisheria utapewa kipaumbele bila kujali kwamba anayetuhumiwa anawadhifa gani katika serikali yangu akituhumia au kupata tuhuma zozote zitafanyiwa kazi kujiridhisha. Pamoja na hayo kinga ya Rais haitikuwepo ili kuhakikisha sheria ndio muongozo halisi katika utawala wangu.
Bado inaendelea........