Controversial
Member
- Mar 8, 2015
- 42
- 6
Hatutaki rais atakae deal na barabara peke yake kwani sisi watanzania tuna mambo mengi kama vile maji,umeme,afya n.k hivyo rais pekee wakututoa ktk matatizo yote hayo ni LOWASSA.
Hiyo ndo machine yenyewe na sasa tunampeleka Ikulu ili aendelee kujenga na nyingine kibao, sahiv Barbara kama unateleza vile
akikamata madaraka patakua kama ulaya ndani ya miezi 6
Ni ile ya kutoka Mtwara mpaka Bukoba kupita katika barabara ya lami. Ni mwaka 2005 alipotoa maneno hayo;
Mkapa na Magufuli mwaka 2005 Jiwe la Msingi Nangurukuru – Mbwemkuru (Lindi) km 95.
Rais Benjamin Mkapa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mwaka 2005 walipoweka Jiwe la msingi Barabara ya Nangurukuru - Mbwemkuru (Km 95). Ujenzi wa barabara hii ulikamilika Januari, 2008.
WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami,hayo yalisemwa Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha Mlata (Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba. Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.
Hata hivyo ahadi ya Magufuli imetekelezwa kwa kuwa sasa barabara yote kuanzia Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.
Serikali ya awamu ya nne imetimiza ahadi ya wananchi ya kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Bukoba imetekelezwa kwa asilimia mia moja (100%).
Barabara, cjui hospital na Huduma nyingine za kijamii n jukumu la serikali. Na kiongozi anayeomba kura kwa hoja za kujenga barabara kwangu mm n sawa na mwanafunzi wa form iv anaandika essay ya civics au n baba anayeomba shikamoo kwa watoto ndo atoe chakula. Tunamtak kiongozi atakayesimamia mgawanyo sawa wa rasilimali zetu ili tupate hizo Huduma za kijamii. Magufuli mfumo ushamkosesha sifa maana atasimamia yaleyale ya hati ya dharura
Tujadili kwa hoja kwani mgombea wenu wa CHADEMA alifanya mazuri yapi akiwa waziri.?