Ndoto ya kufedhehesha.

Escaper

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
1,780
Reaction score
3,241
Nimeota nimezamia kwenye ziara ya mfalme wa kijiji chetu chenye takribani watu mil 50 (ikumbukwe tu mimi si mfuasi wake hata kidogo ) sasa baada ya makofi na vigeregere kutoka upande ule unaomsifu na kumtukuza ukafika wasaa wa mfalme kufunga hafla hiyo.

Gafla akaanza kutoka lile eneo la jukwaa akipita kwenye zulia jekundu,.. kutokana na ugonjwa wake wa KAMERA akajikuta anasimama tena kiasi cha kuwasumbua sana vijakazi wake kuhakikisha usalama wa mfalme.

Huku akipiga selfie na wanakijiji nikaamua japo nichukue selfie moja ya ukumbusho kuwa kuna siku nilipiga picha na mfalme huyo.. sasa katika kupiga picha nikajikuta naweka swaga za vijana kiasi kwamba unabadilisha muonekano tofauti wa vidole nikajikuta nimeweka alama 'V' yani [emoji111]

Daaah aisee nimepigwa sana na wale vijakazi ikabidi niahirishe kuota.[emoji23]

Maendeleo hayana chama!
Asubh njema JF.
 
Duh...... Ina maana pamoja na Mfalme wa hiyo nchi kusisitiza sana kuwa maendeleo hayana chama, lakini wewe kutokàna na kitendo chako cha kuonyesha V uliambulia kipigo??
 
Duh...... Ina maana pamoja na Mfalme wa hiyo nchi kusisitiza sana kuwa maendeleo hayana chama, lakini wewe kutokàna na kitendo chako cha kuonyesha V uliambulia kipigo??
[emoji23][emoji58] hatari mkuu 'V' haitakiwi mbele ya mfalme.
 
Kwanini hukuamua unyanyue dole la kati au halina swaga!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…