Ikawa mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto, na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba, wazuri wanono, walipanda kutoka mtoni, na wakajilisha manyasini. Na tazama ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto . Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto Mara ya pili. Tazama masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki yakatokeza baada hao. Kisha hao masuke membamba saba yakayala Yale masuke saba makubwa yaliyo jaa. Basi Farao akaamka, kumbe ni ndoto tu.
Hiyo ilikuwa ndoto ya Farao mtawala wa Misri , ndoto hiyo ukiangalia kwa makini haina tofauti na maisha yetu hapa bongo.Wa tz tulikuwa na ndoto kubwa sana ya kufikia uchumi wa viwanda, ambao mbali na kuinua uchumi wa nchi ( serikali ) lakini bado ungeinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kwa wale ambao wange pata ajira ktk hivyo viwanda, lkn pia familia zao zinge nufaika kwa kupoza ugumu wa maisha angalau kwa kipato ambacho kinge toka kwa ndugu zao waajiriwa ,kwa kiasi Fulani hii njozi ya viwanda haina tofauti na njozi ya Farao kwa wale ng'ombe saba walionona . Lakini ghafla kukatokea ng'ombe saba waliokonda wakawameza wale walionona. Hawa ng'ombe saba waliokonda ni sawa kabisa na mabadiliko yaliyo kuja ghafla ya kututoa kwenye mawazo ya Tanzania ya viwanda na kumezwa na Tanzania ya kununua madiwani na wabunge wa upinzani , huku tukidhani kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupatikana kwa maendeleo ya haraka, kwani wakosoaji watakuwa hawapo, huku ni kujidanganya, na kujilisha upepo.
Lakini Farao alipo lala aliota tena ndoto ya masuke saba yaliyomea katika bua moja, mema , hii haina tofauti na matarajio tuliyo kuwa nayo kwa kupata mema ambayo yange tunufaisha , lkn ghafla yakatokea masuke saba membamba yaliyo kaushwa na upepo na kuyala Yale masuke saba yaliyo nona , janga linalotokana na gharama za kununua madiwani na wabunge limeleteleza gharama kubwa kwa Taifa hili gharama ambazo zingeweza kuepukwa endapo tu kama busara ungeruhusiwa kutumika, zimetumika mabillioni ya shilingi ambayo yangeweza kujenga angalau hata viwanda viwili vya kiwango cha kati na kuweza kupunguza makali ya uchumi kwa nchi na hata kwa wananchi kwa kupata ajira.
Farao alipo amka toka usingizini agundua kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Viongozi wetu watakapo gundua kuwa kupambamba kuangamiza upinzani kuwa ni kosa kubwa kwa ustawi wa Taifa letu watakuwa wamechelewa kwa hii miaka saba iliyo Baki kwa awamu hii ya tano kukaa madarakani inatakiwa wajitathmini kama kweli wamelenga njia sahihi LA sivyo awamu itakayo fuata baada ya awamu hii kupita itapata tabu sana kuziba mashimo yaliyo sababishwa na ndoto za awamu ya tano.
Amekweli hii ni sawa na ndoto ya Farao na maisha ya bongo.