R_Breazy
Member
- Aug 28, 2025
- 32
- 54
Wakuu habari za asubuhi
Kuna ndoto nimeota zimenitisha sana naombeni msaada wenu kwa atakaezielewa.
Ndoto ya kwanza; nimeota nina chuma mfano wa bolt nakichezea mdomoni ghafla kwa bahati mbaya kikashuka kwenye koromeo, nilhangaika kukirudisha mdomoni hadi nikaamua kuchukua maji nikanywa ili kishuke tumboni sababu sikuwa na namna nyingine.
Ndoto ya pili; nimeota nlikuwa pembezoni/ufukweni mwa ziwa, mwanzo nlikuwa kama nipo mwenyewe ila bada ya muda kidogo mchumba wangu nikimuona (namuita mchumba sababu bado hatujahalalishwa ila tuna watoto 2 hadi saivi) turudi kwenye ndoto.
Baada ya yeye kuonekana pale ziwani, hatua kama 5-6 alionekana ana mtoto wangu wa mwisho, nikawa namuita atoke kana usalama ulikua mdogo sehemu amesimama, akawa anajivuta vuta ila hasogei(muda huo namuita alikuwa ndani ya maji usawa wa magoti kama skosei), aliendelea kumuita kama mara tatu, nikiwa bado namuita mawimbi mepesi yalianza kupiga nkajsogeza pembeni kidogo, kabla sjafika wimbi jingine lilikuwa lishafika nkaguswa na kitu cha ajabu kikawa kinanivuta kuelekea majini.
Nilijitahidi kujitoa kwa kiasi chake nikawa kama nimefanikiwa,ajabu mtu wangu muda wote shirikishi zaidi ya kuomba na kuniita nimsaidie kwenda kumtoa.
Nilijaribu kusogea tu nkamchukue niokoe na mwanangu ghafla nlitumbukia,ilionekana kama chamber ilioko chini ya maji ni kama miujiza fulani kwamba ndani ya chamber kulionekana kuna space ambayo haijajaa maji nilijaribu kurudi kupitia vigape vilivyo kuwa vinaonekana nikashindwa, kusogea nimshike mke wangu nmtoe ghafla nilishikwa na mwanamke ambaye skumfahamu.
Nilijaribu kumkaba ili asimsogelee mtu wangu,ila sikufanikiwa sababu nlijikuta nashika upepo yani hashikiki- sikujua alinigusaje ila ghafla nikawa tu mpole na nguvu alipoteza yaani skufurukuta tena , alipotea ghafla baada ya kitendo kile na ghafla niliona watu wakinifuata kana mfungwa sasa tayari walinichukua mpaka sehemu fulani wakaniacha kwamba wafuate jambo fulani, muda wote wanafanya hivyo akili yangu inawaza kutoroka ila natorokaje ikiwa ile sehemu kulioneka kuna ulinzi mkali na uchawi wa hali ya juu, nlijisemea haya moyoni nikiwa natembea tembea( ikumbukwe huko chini ya ziwa nlikotumbukia hukukuwa na maji ni sehemu ya nchi kavu, ni kama nilifungua mlango wa chumba kimoja kwenda kingine).
Katika kutembea tembea ndani ghafla niliona watu wanapiga kazi nzito na wamechafuka vumbi mfano wa wafungwa (nlijisemea moyoni ina maana namimi nitakuwa kama hao, siwezi lazima ntoke). Niliona gate kubwa kwa mbele nkaona hili ndio njia pekee na nafasi ya kutoka, Sababu nlikuwa sjavishwa nguo za ajabu nlimfuata mlinzi kwa kujiamini na kuomba anifungulie nipite, bahati nzuri nlikuta anaongea na simu, alimuita kijana mmoja achukue ufunguo anifungulie, yule kijana tuliongozana nae taratibu akinipigia story amechangamka ila ile amefungua tu geti kwa haraka nkamuaga ili nisistukiwe, ghafla nilisikia kelele nzuiliwe wa nilitumua mbio na mtu wa kwanza kunifukuza alikuwa ni yule kijana alikuwa mwepesi ila nilikua mwepesi kuzidi,nlikimbia hadi nikaenda kuparamia familia ambayo nilikutana kundi la mbwa kama 20 wakaunga namimi wachache waliobaki wakaunga na yule alikuwa ananifukuza, kundi jingine la watu kutoka ile sehemu nimetoka lilikuwa mbali sana lilokuwa linanifukuza mpaka kizaa zaa cha mbwa kinaisha kundi jingine lilikuwa limeshafika eneo la tukio.
Bahati nzuri nilifanikiwa kutoka kwa wale mbwa hadi nkakimbilia kwenye mpando ambao mbwa walishindwa kupanda. Nlipofanikiwa kuvuka ule mpando kulikuwa na vichaka nlidesh kama naenda mbele halafu nkarudi nyuma nkajificha asilimia kubwa walipitiliza wachache walibakia wakitafuta tafuta eneo nililokuwa nimejificha... ghafla nilishtuka nikiwa na hofu sana
Kuna ugomvi mzito umetokea jana, muda wa kulala ulipofika kabla sjashikwa na usingizi nlirudia haya maneno mara 7 niliomba " Ee Mungu nionyeshe upande mbaya wa mwenza wangu kupitia ndoto usiku wa leo ntakapolala"
NB: ndoto zote nimeota kwa mfuatano ni kama episode 1 iliisha ikaanza 2 na niliposhtuka naangalia saa ni saa moja asubuhi
Natanguliza shukran na mniwie radhi kwa mwandiko na mpangilio mbovu.