Ndoto Kuhusu Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto Kuhusu Afrika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TANURU, Mar 6, 2010.

 1. T

  TANURU Senior Member

  #1
  Mar 6, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikiwaza sana ni kwa jinsi gani tunaweza kuliunganisha bara letu la Afrika kwa gharama nafuu kabisa na kuweza kuwa na fursa ya kuweza kuona na kujua kila siku nini kinafanyika katika nchi zetu.
  Tunakuweza kweli kuungana kisiasa lakini bila ya kuwa na Televisheni Yetu Maalum ya Afrika ambayo itaonekana katika kila kijiji hapa Afrika, basi tutaendelea kuota ndoto za mchana kila siku. Televisheni hii itatusaidia sana katika kukuza demokrasia na kujifunza mambo mbali mbali toka katika nchi zetu na itakuwa pia rahisi kuwa na mafunzo maalum kwa njia ya Televisheni yakilenga zaidi katika kutuongezea ujuzi na maarifa katika nyanja mbalimbali lengo kuu likiwa ni kufuta umasikini katika uso wa bara letu ndani muda usiozidi miaka 30 toka sasa. Ni muhimu sana Televisheni hii iwe na Channels zaidi ya Tano ili kuhakikisha kuwa matangazo yake na mafunzo kupitia Televisheni hii yanapatikana kwa lugha zote kuu zinazotumika katika bara letu. Itakuwa pia rahisi kuwaunganisha wataalam wetu mahili walioko ndani na nje ya bara zetu la Afrika kupitia Televisheni hii (PAN AFRICAN TELEVISION---PA TV).
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...