Ndoto inayonitesa maishani

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,651
Amani iwe juu yenu.

Ndugu zangu nimekuwa na ndoto ambayo imekuwa ikinitesa sana katika maisha yangu,

Ni ndoto ya kutamani siku moja nimiliki kampuni ya UOKOAJI katika majanga mbalimbali isipokuwa majanga ya moto.Majanga ninayoyakusudia hapa zaidi ni ajali za Barabarani pamoja na zile za Majini bila kusahau ajali zingine km za treni,majengo n.k

Ndoto hii nakumbuka iliibuka ghafla kipindi kile ilipotokea ile ajali ya treni Dodoma katika vile vijiji vya Msagali sikumbuki na kijiji gani ila wote tunakumbuka iliua maelfu ya ndugu zetu.Iliendelea kunitesa pia zilipotokea zile ajali 2 za meli za kule Nungwi za MV Skagit na Spice Islander bila kusahau matukio ya ajali za barabarani ambazo zinachukua maisha yetu kila uchao.

Ni kweli tuna jeshi la zimamoto na uokoaji ila kiukweli nadhani limeelemewa na bado linafanya kazi kianalogia/Kizamani mno hali inayopelekea watu wengi katika ajali huwa kwa kukosa msaada wa oukozi wa haraka.

Ndoto hii inanitesa kwa kuwa inahitaji investment/Uwekezaji ambao nashindwa kuelewa kama nitakuja kuufikia mpaka naondoka ktk dunia hii maana ninahisi nitahitaji vifaa vya mabilioni km ifuatavyo
--Helicopter walau 2 always standby
--Heavy Crane motovehicles walau 4 ziwepo katika kanda 4 za nchi hii.
--Boti ziendazo kasi walau 5 zigawanywe katika maziwa na baharini.
--Vifaa vya Kisasa vya kukatia vyuma vigumu.
---Jeki zenye uwezo wa kunyanyua vitu vizito sana na za kisasa.
--Well tranned Resque squad.
Vingine vi naweza kuwa vya kawaida.

Kutokana na picha ya hiyo investment nalazimika kuendelea kuuumia na hakika naweza kufa nikiwa sijaitimiza ndoto yangu hii na kinachouma ni pale unapobahatika kupata nafasi ya kufika katika eneo la ajali na KUMSHUHUDIA MTU ALIYEBANWA NA VYUMA AKIKUOMBA MSAADA UMUOKOE HUKU AKIKUAHIDI KUKULIPA HATA KILE ASICHOKUWA NACHO ILI MRADI TU UWEZE KUMUOKOA ila kwa kuwa huna uwezo basi unashuhudia pia hadi mtu huyo anakata roho mbele yako,hakika niliwahi kuuumia kwa hili.

Tafadhalini ndugu zangu naombeni japo mawazo kidogo namna gani hata naweza kuliweka katika maandishi tu at least nijue niliwahi kujaribu kitu hili katika uhai wangu japo nilikwama kutokana na uwezo wangu licha ya kuwa naamini hakuna kisichowezekana chini ya jua.

Wenu BACHELOR SUGU.
 
Achana na ndoto mkuu. Amka kutoka usingizini, Weka mikakati katika malengo madogo madogo yanayo tekelezeka, kuwa na uthubutu. Fanya
 
Mkuu hata hapa tayari umeliweka kwenye maandishi...ni wazo zuri watalisoma na wengine...huenda kuna mtu atalitumia
Yeah ni kweli mkuu mwenye uwwezo wa kulitumia alichukue tu atakuwa amenisaidia kulifanyia kazi
 
kwa kuwa umeomba hata ushauri tu,basi jitahidi uanzishe kampuni ya kuwagundua wasiojulikana.
 
Sikukatishi tamaa, ila kuwa muokoaji kwa nchi ya kubwa kama Tz, hizo namba za vifaa hata kwa wilaya unaweza usifanikiwe licha ya kwamba ajali hazitokei kila siku.
 
Nimevyoona kichwa cha uzzi tu nimeogopa kuufungua

Ukizingatia usiku huu
 
Nimevyoona kichwa cha uzzi tu nimeogopa kuufungua

Ukizingatia usiku huu
Pole sana mkuu,lakini si umefunga mlango?Ok umeshaufungua wazo lako laweza kuwa muhimu
 
Mkuu una uhakika kwamba hii ndoto yako hujirudia kila unapolala?
 
Science and technology ni tatizo kwa nchi za Africa especially Tz.

Nionavyo mimi, wazo lako linaweza kufanikiwa vizuri zaidi kama tungekuwa katika atleast level ya utumiaji wa cctv cameras barabarani na sehemu zote za miji. Hii inasaidia kutrace kwa haraka matukio na kufika kwa wakati.

Ushauri: Hauhitaji kuwa na ivestment kubwa sana. Wazo lako ni investment tosha kabisa. Kinachotakiwa wewe uushinde woga na uanze pale unapoweza. Mfano, tafta pesa kidogo na uanze na mji mmoja mfano Dar es salaam ambako kuna watu wengi lakini pia matukio ni mengi. Na unapoanza anza na kitu kimoja mfano, uokoaji majini tu na unaweza anza na uokoji kwa wanaoogelea tu, ukaweka vijana ambao wako competent kwenye kuogelea na wanavifaa vya kuokoa majini. Na unakuwa katika sehemu zile za beach zenye watu wengi. Hii itakusaidia kutambulika na mamlaka huska lakini pia utendaji wako ukiwa mzuri ni rahisi kupata investors kwa yale mengine unayotamani kuyafanya.

Inawezekana, anza leo.

Kwa ushauri zaidi, njoo pm.
 
We jamaa umenigusa aisee yaani umenipa nguvu kwa ushauri huu mpaka nimehisi ninaweza kufanikiwa ndoto yangu.Nakuja Pm mkuu,ubarikiwe sana.
 
Dah, jf tungekuwa angalau na robo ya watu wenye mawazo mazuri kama yako tungefika mbali sana
Dah mkuu tuendelee na maombi tu ipo siku tutaongea lugha moja japo sijui itachukua muda gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…