Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,536
Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya shauri la Kikatiba la kupinga Vifungu vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18
Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, jana Tarehe 8/7/2016 imetamka kuwa vifungu vya sheria ya ndoa namba 13 na 17 vinakauka Katiba na kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuoa/kuolewa. Mahakama Kuu pia imeipa serikali maagizo chini ya mwanasheria mkuu wa serikali, kuwa imeshabadili hii sheria ndani ya mwaka mmoja na kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini kwa msichana na mvulana kuolewa/kuoa.
Kesi hii ya Kikatiba iliyosajiliwa na kupewa namba 5 ya mwaka 2016 ilifunguliwa na Rebeca Gyumi, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative,linalofanya kazi ya kutetea haki ya mtoto wa kike kupata elimu,kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocates.
BOFYA: HUKUMU YA MAHAKAMA
Zaidi, soma;
Serikali yaanza kupinga hukumu Sheria ya Ndoa kwa watoto wa kike juu umri sahihi wa kuolewa

Rufaa ya Serikali kutaka watoto waendelee kuolewa wakiwa na miaka 14 yatupiliwa mbali
Uamuzi huo unamaanisha kuwa mtoto wa kike na wakiume anapaswa kufikisha miaka 18 ndipo aweze kuingia katika maisha ya ndoa. Kesi hii ilifunguliwa na mwanaharakati Rebecca Gyumi Kesi hii ilifunguliwa kwa msingi kuwa vifungu hivi vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 vimepitwa na wakati na kandamizi...
www.jamiiforums.com