Ndoa za Kanisa Katoliki

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
460
Reaction score
1,411
Habari za huku,

Nimebahatika kuhudhuria ndoa mbili za kanisa katoliki, nimeona siku hizi neno “KATIKA SHIDA NA RAHA MPAKA KIFO KITUTENGANISHE” halitumiki tena.

Hii inaashiria nini? Ndoa za kanisa katoliki mnaruhusiwa kuachana kikanisa au divorce rate imezidi kua kubwa hivo hamna umuhimu wa kutumia maneno hayo?
 
Hicho kiapo ni kama "vision" hivi!
So kunatakiwa "mission" kukamilisha vision.

Mission ikikwama vision inapotea. Wenyewe wanasema kufanikisha haya nguvu ya Mungu inahusika.
 
Akya mungu tena sijaelewa
 
Soma tena andiko la mleta mada halafu linganisha na lako kisha tuoneshe maneno "HADI KIFO KITAKAPOTUTENGANISHA".
Kupenda na kumheshimu mtu ni simple tu unaweza hata kumheshimu Mzazi mwenzio.
 
Wewe jamaa unataka kupotosha umma! Ndoa ya kikatoliki ni noma. Ni kifo tu ndiyo hutenganisha wana ndoa. Mkiachana kabla ya hapo, basi utafunga ndoa kanisa lingine, ila siyo katoliki.

Na ukitumia ujanja ujanja na ikigaundulika tayari ulishakuwa kwenye ndoa hapo kabla, ndoa hiyo mpya hutenguliwa mara moja. Katika jambo hili, Kanisa Katoliki halina utani kabisa.
 

Soma vizuri uelewe swali
 
Bado kuruhusu wanaume kuwa na mke zaid ya mmoja na padri nae aowe .

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Naunga mkono hoja. Hayo mambo mawili yametufanya Wakatoliki tuishi maisha ya kinafiki sana. Baadhi ya Mapadre wanaoshindwa kuishi maisha ya kiseja, wamejikuta wakinogewa kiasi cha kuwa na watoto wa kutosha tu kwa SIRI!

Ukija kwa sisi wanaume ndiyo usiseme! Wengi wetu tuna nyumba ndogo za kutosha tu!! Bora tungeruhusiwa ili unafiki upungue.
 
Kweli mtihani waweza kuwa mrahisi tena ni wa 'kushedi' kama wa darasa la7 lakini mtu unakuta anafeli kimasihara!

Mfano huo nimeutolea kwenye comment yako hii, je mtoa mada kauliza swali gani na wewe umejibuje?
 
Soma vizuri uelewe swali
Sasa mbona hapo hakuna swali!! Yaani inawezekana ulikuwa ni msinziaji mzuri wakati unahuduria hizo harusi au hukuwa unasikiliza kwa umakini kinacho endelea hapo kanisani kwa sababu zako binafsi.

Hayo maneno hayawezi kutolewa bila sababu za msingi. Na ndoa za kikatoliki bado zina nguvu ile ile! Na hata idadi ya hao wanandoa wanao achana binafsi nadhani ni ndogo sana ukilinganisha na ya wale wanao komaa mpaka mwisho.

Hivyo upotoshaji kwenye hii mada yako, kubali tu haukwepeki!
 
Wewe ulikuwa unasinzia kanisani.
Kiapo cha kanisa katoliki hakijabadilika.
Nenda kasome tena Miongozo ya kanisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…