Ndoa yangu iko njia panda

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,779
Reaction score
1,227
Yaani imekuwa shida sasa mpaka najilaumu kwanini mke wangu niliamua kumnunulia smart phone.

Takriban miezi mitatu imepita toka nimnunulie simu aina smart kwa nia njema tu kutokana na kazi ya kuuza duka muda mwingine wateja hamna basi aitumie tu ku-refresh mind, lakin kadili siku zinavyokwenda naona hali inabadilika yaani amekuwa adicted mpaka majukumu yake anamwachia house girl wakati zamani haikuwa hivyo, juzi kati hapa nilitembelewa na mama yangu nae alishangaa kumkuta mkwe wake amebadilika yaani si kama zamani walikuwa wanapiga stori na kufurahi pamoja lakini saa hizi wanaweza kukaa sebureni pamoja zaidi ya saa nzima hata bila ya kuongea na hata akimuongelesha hujibiwa majibu ya mkato baada ya hapo mtu yuko na bizy na chart 'atih mwana umo mu simu kuna nini mpaka mtu acheke peke yake au atabasamu au akunje sura ghafla' swali ambalo aliniuliza mama kimzaha lakini sikumjibu ila moyoni niliumia sana.

Sasa nimeanza pata malalamiko toka kwa wateja kuwa 'mke wako siku hizi anajisikia sana sijui sababu ana vitz nilipitia dukani kwako kumuulizia vitenge vya wax akanijibu kimkato na kuwa bisy na simu wakati sio kawaida yake.

Jana usiku nilishtuka majira ya saa 8 nikakuta anachat nikamuuliza kwanini inakuwa hivyo akajibu hana usingizi
leo asubuhi nimemwacha anapika mswaki kufika ofisi nikafungua acc yangu ya fb nikakuta status yake ya habari za asubuhi wapendwa yenye like 57 na comment 35 na picha akipiga mswaki.

Sijui kama jf hapa yupo lakin sheeda na talaka inanukia
 
Dah.......huyo mkeo ipo kazi........mweee.....
 
apana, nakuomba usimuache kwanza, muelimisha, mpe elimu ya ziada juu ya mambo ya kiteknolojia, mfahamishe, mtishie, kakamaa, wew ni m.mme mnyooshe mkeo,
akishindikanwa msukumie talaka, na aende akaolewe na smart phone
 

umeoa lini ??
story zako hazina series nzuri

ha ha ha ha ha ha ha ha

shule umemaliza lini dogo ?
 
Mke wako alikuwa amelala, ukamuasha. Itabidi tu ujifunze kuishi na hayo makitu ya smart.
 
Teh
Ni ulimbukeni tu huo!!!!!

Jaribu kumueleza kwanza kabla hujafanya maamuzi !!!!
 
Ni wewe na ndugu zako kujipanga ili muwe na maneno matamu zaidi ya fb na whatsapp ili awarudie.
 
umeoa lini ??

story zako hazina series nzuri


ha ha ha ha ha ha ha ha


shule umemaliza lini dogo ?

Hahahaaaa duuuh...hatare af kinaonekana kindugu changu hichi lkn kina mambo ya ovyo hadi sijakipenda
 
Hahahaaaa duuuh...hatare af kinaonekana kindugu changu hichi lkn kina mambo ya ovyo hadi sijakipenda

Watu wamemdukua, hii inabore sana. Kuna watu wanaumiza vichwa kutoa ushauri kumbe story ya kutengenezwa halafu mtu kajivika uhusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…