Ndoa ya ccm na cuf yatoa raisi ukawa

Mchafuzi

Member
Apr 24, 2008
45
21
Jana Wadanganyika walipatwa na butwaa baada ya kushuhudia mazingaombwe ya CCM yaliyofanywa Zanzibar yakijirudia tena kwa Watanganyika kwa kuibua ndoa ya CCM na CUF kiaina.Ndoa hii iliyosababisha Maalim Seif arejeshewe mafao yake na hatimaye kuwa makamu wa rais kwa upande wa Zanzibar, sasa imetengenezwa tena kwa upande wa Tanganyika ambapo mgombea toka CCM na Makamu wa mwenyekiti wa CUF wamepitishwa kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA. Wagombea hawa ni Edward Ngoyai Lowasa toka CCM na Juma hajji Duni toka CUF. Wote kwa pamoja wamejivua uanachama wa vyama vyao na kutumia chama cha CDM ambacho Watanzania wengi walikwisha kiamini kama ndiyo mkombozi wao ili wapate ridhaa ya kuwania uraisi wa Tanzania. Haya ndiyo mazingaombwe ya CCM yaliyofanyika visiwani na sasa yamehamia bara. Edward Lowasa ambaye hajawai kufanya kazi mahali popote zaidi ya CCM toka amalize chuo ndiyo CDM wameona anaweza kupeperusha bendera ya UKAWA akishirikiana na Juma Hajji Duni toka CUF.Hii inamaanisha kwamba chama makini CDM hakikuwa na mgombea ambaye anaweza kuongoza nchi hivyo wao wanajipanga kushika majimbo kwa viti vya ubunge tu lakini uraisi wanawaachia CCM na CUF. Edward Lowasa nadhani ana mpango wa siri kuua upinzani nchini kwani nashawishika kusema mtu huyu ni hatari sana tena aweza kuwa ni “trained Jasusi” ambaye amepandikizwa na CCM upande wa upinzani ili hatimaye upinzani upotee na CCM iendelee kutawala daima dumu. CUF wao hawana hasara yoyote kwani hata kama EL ataingia madarakani wao watapeta tu kama wanavyopeta visiwani kwa kula bata kama makamu wa raisi, hasara itabaki kwa watanganyika ambao wamejtahidi kwa zaidi ya miaka 20 kuunda upinzani wa dhati ambao unasambaratishwa kwa urahisi kabisa nadhani ili ndilo Dr.Slaa kaliona na kuhamua kujiweka pembeni ili ikiwezekana mara baada ya uchaguzi ahanzishe harakati za kufufua upinzani tena kwani kaona watanzania hawata waamini tena watu wanaoitwa “wapinzani”. SOMO: Chama kilichokua kikionekana kama mkombozi wa kweli CDM kumbe hakikuwa kimejitayarisha kusimamisha mtu ambaye angewagalagaza CCM na kukiondoa madarakani zaidi ya kushika viti vya Ubunge USHAURI: tutakapoanza upinzani wa kweli mara baada ya uchaguzi wa Oktoba tutafanya mapitio ili tusijehujumiwa na CCM kama walivyotumaliza 2015, kwako Dr. Slaa ni wakati sasa wa kutafakari jinsi ya kuibua upinzani wa kweli na haya mapandikizi toka CCM tuwe nayo macho. Kauli ya jana ya JK pale ofisi ndogo ya CCM Lumumba kuwa watashinda uchaguzi ni ya kweli kwani hata EL akishinda si ndiyo mpango wao!!
 
Back
Top Bottom