Ndoa ya bomani

Samahani wanajamii wa Tz, naomba kuuliza kama kuna mtu anafahamu, JE naweza funga ndoa ya bomani na mtu asie mtanzania!!
Inawezekana kabisa.
Ndoa zote za kanisani, Misikitini na serikali(Bomani) zinasajiliwa na RITA kwa Mjibu wa sheria ya Ndoa Na. 5 ya mwaka 1970
 
Anzia kwa DC utapata maelekezo yote mkuu. Hongera kwa kumbahatisha huyo shemeji yetu.
 
inawezekana vizuri tu, nenda ofisi ya mkuu wa wilaya unayoishi, kuna taratibu zake simple tu.
 
Samahani wanajamii wa Tz, naomba kuuliza kama kuna mtu anafahamu, JE naweza funga ndoa ya bomani na mtu asie mtanzania!!

Ndiyo ndoa rahisi zaidi ya yote. Fika kwenye ofisi za wilaya utoe taarifa ukiwa na viambatanisho vya msingi kama Certificate of no impediment marriage kwa huyo mtarajiwa wako au document inayoonyesha ni divorced.

Tangazo linachukua siku 21 ngoma inafungwa kiulaini unahitaji tu mashahidi wawili tu haina mbwembwe na inalinda mfuko wako hasa ila kama unataka pia kuuza sura unaweza kuandaa sherehe baada ya hapo.
 
Inawezekana kabisa.
Ndoa zote za kanisani, Misikitini na serikali(Bomani) zinasajiliwa na RITA kwa Mjibu wa sheria ya Ndoa Na. 5 ya mwaka 1970
Hivyo kaka natakiwa kwenda Rita kwanza au moja kwa moja kwa DC!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…