Ndoa tamu

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Jamaa yangu wa FB amesema hivi:

Ndoa haibadilishi tabia ya mtu,nyie ambao mna hopes kwamba aah my boy atabadilika tu huko mbeleni tukioana,or my girl atabadilika,habadiliki ng'oo!
Kama anakupiga ngumi leo be sure atakutandika na mwiko huko ndani...Ukikosea kudhani kwamba Ndoa inakuja na changes utapotea.

Ndoa inakupa pete tu kidoleni na kukuchange title,ila sio tabia.Kama anapenda dagaa leo ndoa haitambadilisha apende matembele.Make the right choices leo lasivyo utakuwa mtumwa wa tabia zake milele.

Kosa kubwa watu hufanya ni kuamini kwa sababu ameamua kuniweka ndani,haya mambo yatakuwa madogo na with time atachange,HAPANA!
Kamwe usithubutu kufanya Assumptions na ndoa,tabia ya mtu kwenye ndoa itaonekana Mapema,huwezi kuona Jua linawaka halafu uwaambie watu sasa
hivi ni Saa3 usiku,utakuwa Kichaa.

Ni muhimu kufanya maamuzi sahihi,kwenye muda sahihi,na kwa mtu sahihi,la sivyo,ndoa haitakuwa chaguo sahihi kwako,utajikuta umejifunga
kwenye Mateso ya milele!
 
Kwanini ukosee. Kaaa ma mtu kwa muda mwingi utaelewa
 
Mlio kwenye ndoa njooni jamani, we need proof of these words..!!!
 
Neno ndoa liacheni kama lilivyo,raha ya ngoma uingie ucheze,kila siku mtaambiwa mengi, kuna magood pretenders ni

malaika sana before marriage after marriage ndo utawajua vizuri, BTW kila mtu ana ndoa yake kuna mazuri yake na

mabaya yake,mabaya yako ndo mazuri yangu na mazuri yangu ndiyo mabaya yako.
 
Tabia kama ngoziii aisee ni ngumu kuibadilisha
 
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…