Ndoa ni kitu kizuri sana pamoja na changamoto zake.

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
904
1,399
Habari za saa hizi wakuu,ni matumaini yangu mko salama kabisa na mambo yanaenda salama kabisa.

Leo nimeona itakuwa vyema tukikumbushana mazuri ya ndoa japo kidogo baada ya kuona threads kadhaa za siku hizi zimejikita kwenye changamoto za ndoa pekee huku baadhi zikienda mbali na kusifia michepuko.

Bila kukumbushana mazuri ya ndoa tuliobahatika kuwa katika ndoa tutaacha uongo WA ubaya WA ndoa usemwe sana na hatimae uaminike kuwa ndio ukwel na kuwakatisha tamaa wanaotaka kuoa.

Binafsi nimeoa na nafurahia ndoa yangu na haya ni baadhi tu ya mambo yanayonifurahisha ktk ndoa.

1. Utulivu WA nafsi.
Tuacheni masikhara mapenzi Yasio ya ndoa Yana stress nyingi sana,binti au kidume kwakuwa hajajihakikishia kuwa wewe ni wake jumla huwa anakuwa mguu ndani mguu nje,matokeo ya Hilo ni michepuko na kuumizana moyo.lakini ukioa moyo unatulia kila mmoja anajitoa kwa asilimia zote kwa mwenzake na furaha inatawala.

2. Mapenzi ya dhati
Kule nje ya ndoa ni vurugu tupu,huyu anakutaka kutuliza nyege zake tu,yule anakutaka ili akuchune visenti vyako navurugu nyingi baada ya malengo ya wahusika kutimia unamwagwa Bila huruma,kwenye ndoa mapenzi ni ya dhati uwe nacho au usiwe nacho mwenzi wako upendo ni palpale,umpe leo umpe kesho upendo palepale katika shida na raha.

3. Mipango ya maendeleo
Kiukweli sio rahisi sana mtu na boyfriend wake kukaa wakapanga Mipango ya maendeleo kwa ajili ya future,sio kwamba hawapo watu WA Aina hiyo ila ni wachache mno,mahusiano ya nje ya ndoa huwa Mara nyingi yanajikita kwenye mapenzi tu.katika ndoa majadiliano ya namna ya kuboresha kipato cha Familia huwa yapo kwa faida ya faida ya Familia,haya hupelekea kutanuka kwa mawazo na kuongezeka kwa bidii ya utafutaji na hatimae maendeleo hupatikana.

4. Baraka
Ndoa huvutia Baraka na rehma za mwenyezi mungu kwa wahusika hasa kwakuwa tendo LA kuoana ni tendo jema linalohimizwa na dini zote. Hii huwasaidia sana wanandoa kuboreka kimaisha kutokana na kufanikiwa hata ktk utafutaji Wao.

5. Kujaliana
Mapenzi ya ndoa hugubikwa na upendo WA Kujaliana kwa wawili walio ktk ndoa,mmoja akiumwa ni huzuni na mashaka kwa mwengine na huangaika kweli kuhakikisha mpaka mwenza anakuwa Sawa,kwenye mapenz ya nje huko huchelewi kutelekezwa ukiumwa na kutafutwa ukipona.

6. Heshima
Walio katika ndoa tunainjoy Heshima kubwa tunayopata kuanzia kwenye Familia zetu na jamii kwa ujumla kwa tendo Hilo LA Heshima kubwa LA kuwa katika ndoa,hii ni tofauti kwa asie ktk ndoa ambae anaweza kuonekana muhuni tu.

Hayo ni baadhi tu ya mazuri yaliyo ktk ndoa,walio ktk ndoa karibuni tuchangie ili kufuta tuhuma nyingi zinazoelekezwa ktk taasisi yetu hii na tuwape moyo ambao hawajaingia.
 
Ndoa ni kizungumkuti, waliopo wanataka kutoka ambao hawapo wanatamani kuingia
Ni kama embe... wakati wengine wakisubiri liive, wengine wanalitia chumvi wanalila likiwa bichi.
images
 
Mkuu mtoa mada nakuunga mkono kwa kutupa hoja yenye mtizamo tofauti at least sio kila siku malalamiko tuu ya ndoa.
 
Back
Top Bottom