Ndoa ndoano, nani tatizo?

Ndoa ndoano, nani tatizo?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,168
Reaction score
48,446
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanaume wengi huingia kwenye ndoa bila ya kutarajia, wakati wanawake ni moja ya mipango yao ya maisha tangu wakiwa washichana wadogo. Kwenye ndoa wanawake wanakuwa na mipango tofauti sana na wanaume.

Ni nani hasa kati ya mwanamke na mwanaume ambaye anasababisha hadi ndoa ionekane ni taasisi yenye dhahama nyingi kuliko raha?
 
Jibu la mkato:

Mwanamke.

Maelezo mafupi:

Mwanamke amehama kutika kwao kwenda mji mwingine, ana wajibu wa kueneda kama mazingira mapya yanavyomtaka kufanya.
Sasa yeye anaona kmnyenyekea mme ni utumwa.
 
Jibu la mkato:

Mwanamke.

Maelezo mafupi:

Mwanamke amehama kutika kwao kwenda mji mwingine, ana wajibu wa kueneda kama mazingira mapya yanavyomtaka kufanya.
Sasa yeye anaona kmnyenyekea mme ni utumwa.
Mwanamke hajaumbwa kwa ajili ya kumnyenyekea mwanaume..

Amuheshimu mwanaume kama mume wake na mume amheshimu mwanamke kama mke wake..

Ndoa ni taasisi ambayo wanandoa wote wawili wanawajibika sawa katika kuipa ustawi imara.
 
you have been awarded 1 trophy🙂
 
Patience123 inavoonekana ni kama vile wanaume wengi hulalamika kuwa wanawake hutaka kuyageuza matamanio yao ndiyo yawe matamanio ya ndoa yao. Kwa mfano wanaume wengi huweza kuishi kwenye nyumba yoyote ile ya kupaga, lakini wanawake wako bize mara nyingi kukosoa uchaguzi wa nyumba watakayochagua mwanaume kupanga!!
 
Mwanamke hajaumbwa kwa ajili ya kumnyenyekea mwanaume..

Amuheshimu mwanaume kama mume wake na mume amheshimu mwanamke kama mke wake..

Ndoa ni taasisi ambayo wanandoa wote wawili wanawajibika sawa katika kuipa ustawi imara.
Taasisi yoyote ina majukumu na lazima iongozwe.. kila binadamu hapa duniani ameumbwa kwaajili ya kazi fulani na ana majukumu yake katika jamii, familia, kazini, kitaifa na kwengineko ila pia kila mmoja ana nafasi yake katika NDOA.. iwapo wewe ni muumini wa dini eidha ya kikristo ama ya kiislam.. Mie mkristo na dini yangu inaagiza hivi mwanaume ampende mkewe kama Yesu alivyolipenda kanisa.. amlinde na kumhudumia mkewe.. n.k. mwanamke aliambiwa awe mnyenyekevu na amuheshimu mumewe.. haya majukumu Mungu aliyaweka kwasababu nyingi ila kwa msingi huu Ndoa inaweza kuimarika mambo mengine yanapoingia tu.. Ndoa lazima ivurugike..
 
lowestein inaaminika siku hizi wanaume hawatimizi majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha ndoa nyingi kusambaratika!
 
Mwanamke hajaumbwa kwa ajili ya kumnyenyekea mwanaume..

Amuheshimu mwanaume kama mume wake na mume amheshimu mwanamke kama mke wake..

Ndoa ni taasisi ambayo wanandoa wote wawili wanawajibika sawa katika kuipa ustawi imara.
Unyenyekevu ni sehemu ya heshima!
Kama nimekosea lugha hiyo sawa, nipe ANDIKO linalomtaka "mume kumheshimu mke"
 
Unyenyekevu ni sehemu ya heshima!
Kama nimekosea lugha hiyo sawa, nipe ANDIKO linalomtaka "mume kumheshimu mke"
Lakini kuna baadhi ya wanaume badala ya kuheshimiwa wanataka waabudiwe bila ya wao kutimiza kwanza majukumu yao ya kiuanaume!
 
Tatizo ni mwenye tatizo.

Awe me au ke alieyesababisha vitu vikaenda mrama ndiye tatizo.

Kuna wanawake wapo focused lakini pia kuna wanaume wapo focused
 
Jibu la mkato:

Mwanamke.

Maelezo mafupi:

Mwanamke amehama kutika kwao kwenda mji mwingine, ana wajibu wa kueneda kama mazingira mapya yanavyomtaka kufanya.
Sasa yeye anaona kmnyenyekea mme ni utumwa.
Ongeza na hii, mwanaume kabla hajaoa anashida zake tu, baada ya kuoa shida za mke na wakwe zote zinakuwa zake na stress zamke anabeba pia
 
Mwanamke hajaumbwa kwa ajili ya kumnyenyekea mwanaume..

Amuheshimu mwanaume kama mume wake na mume amheshimu mwanamke kama mke wake..

Ndoa ni taasisi ambayo wanandoa wote wawili wanawajibika sawa katika kuipa ustawi imara.
Mwanamke inatakiwa amheshimu na kumtii mme wake, bali mwanaume inatakiwa aishi na mke wake kwa akili
 
Mwanamke ni tatizo.

Anapotezwa na miluzi mingi.
Anapenda kuwa kama fulani wakati uwezo ni mdogo sana na anajisahau mapema mno.
 
Patience123 inavoonekana ni kama vile wanaume wengi hulalamika kuwa wanawake hutaka kuyageuza matamanio yao ndiyo yawe matamanio ya ndoa yao. Kwa mfano wanaume wengi huweza kuishi kwenye nyumba yoyote ile ya kupaga, lakini wanawake wako bize mara nyingi kukosoa uchaguzi wa nyumba watakayochagua mwanaume kupanga!!

Mkuu hapa inategemea na kuwa umeoa mke wa daraja gani/hadhi gani. Kama umeoa Kutoka daraja la juu na uwezo wa kumhudumia kuendana na daraja Lake huna, hayo ni lazima yatokee. Mtu achague mke kuendana na hali yake.
Unyenyekevu ni sehemu ya heshima!
Kama nimekosea lugha hiyo sawa, nipe ANDIKO linalomtaka "mume kumheshimu mke"
Mkuu hapa tupo kwa imani tofauti,ukisema habari ya maandiko huenda tusielewane. Labda tubaki na hilo neno" heshima "

Kwenye ndoa kila mmoja anapaswa kumheshimu mwenza wake
 
Ha
Mwanamke ni tatizo.

Anapotezwa na miluzi mingi.
Anapenda kuwa kama fulani wakati uwezo ni mdogo sana na anajisahau mapema mno.
Ha ha ha miluzi mingi hupoteza mwelekeo wa mawindo ya mbwa!
 
Siyo na kwa mwanamke pia shida za Mumewe na wakwe zake nazo huwa zake?
Mwanamke wa hivyo sijamuona labda jimama linaloishi na marioo ila kwa wanaume yapo, tatizo kidogo tu mke anataka hela atume kwao yaani kuoa ukoo maskini ni balaa la kujitakia
 
Sasa yeye anaona kmnyenyekea mme ni utumwa.
Wakunyeyekewa ni mungu.Mume anaheshimiwa.

Jibu langu ni mwanaume.
Sababu, wanaume wengi hawatumizi majukumu yao,wanaona wakishaoa wamemaliza km ni mke atamkuta tuhapo nyumbani,so hajiongezi kwa chochote.
 
Mwanamke wa hivyo sijamuona labda jimama linaloishi na marioo ila kwa wanaume yapo, tatizo kidogo tu mke anataka hela atume kwao yaani kuoa ukoo maskini ni balaa la kujitakia
Na Kwa maelezo ya Patience123 ni kwamba ni vizuri kuoa mtu mnayelingana naye kipato au utakayemudu kushughulika na matatizo yake!!
 
Back
Top Bottom