Ndoa naigopa sana!

Nakuunga mkono mkuu, sijawai ona faida ya ndoa. Zaidi lazima upande mmoja uunyonye mwingine
 
Kwani kazi ya ndoa ni ipi hasa wakuu....πŸ™„
Situlisha kubaliana kwamba ndoa ni kaburi ama...πŸ€’
 
Jifunze kutokuogopa jambo ambalo hujalpitia maishani. Ukiambiwa haya maji ni barid sana bila kuhakikisha hutaoga. U are lucky umeona mabaya mengi kwa upande wa ndoa kumaanisha ukiamua kuingia utakua na uwepesi wa kujua nikifanya hili litaleta mgogoro baina yako na mwenzako. Wewe umeamua kujikopesha uoga na ndio utakutesa. Acha kujimilikisha uoga na unaweza kuwa mfano mzuri kwa wanandoa.
 
bora usela tuh ngoma hiyo siewez
 
Namshukuru Mungu, saizi nina miaka 4 kwenye ndoa. Nimeoa nikiwa na miaka 25.

Ukipata mwanamke wa Kibena Njombe sio wasubufu. Ni wachapakazi balaa.
 
Hata Magari kila siku yanapata ajali na watu wanakufa,

So,usipande gari pia.
 
Naomba kujua faida za ndoa ambazo mtu akiwa hana ndoa hapati
1. Usalama na utulivu wa kihisia
2.Kufisha ubinafsi na kuimarika zaidi katika kuiona thamani ya wengine
NB
Hayo hupatikana tu kwenye Ndoa iliyojengwa juu ya Mwamba na sio juu ya mchanga
 
Ingia google halafu search "Motivated Reasoning" halafu husianisha na uzi wako, itakusaidia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…