Nnakujibu kiuzoefu.
Mwanamme/ mwanamke raia wa kigeni kama alipata uraia wa TZ kupitia mwanamme/ mwanamke ana uamuzi wa kurudi kwenye uraia wake au kuendelea kuwa mTZ, huo mpira unakuwa kwenye wigo wake.
Kama wakiachana huyo mwanamke/ mwanamme ataendelea kuwa raia wa Tanzania kupitia utaratibu wa kuasiliwa uraia au "naturalization" ambao aliuomba mlipooana.
Lakini anaweza kufutiwa uraia huo na waziri wa mambo ya ndani ambae itatokea ameridhika kwamba raia huyo amevunja sheria kwa kuwasilisha pamoja na maombi ya uraia, vyeti vya kughushi au uongo mwingine wa kutunga ili kujipatia uraia wa Tanzania na hiyo ni kupitia sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995 na ile ya 1997.
Pili, kwa kuwa Tanzania hairuhusu uraia pacha basi raia huyo wa kigeni atatakiwa kuukana uraia wa nchi alikotoka na kama atafutwa uraia wa Tanzania basi atapaswa kurudi nchini mwake na kuondoka nchini Tanzania mara moja maana atakuwa anayo passport ya nchi yake (kumbuka akiomba uraia anapeleka copy tu ya pasi).
Nadhani ntakuwa nimekupa mwanga.