Wandugu naombeni ufafanuzi/elimu kuhusiana na hili. Iwe kwa experience ama taaluma, ntashukuru kupata majibu.
Kuna mama mtu mzima aliolewa ndoa ya kanisani miaka mitatu iliyopita. Alikuta mume ana kila kitu (mashamba, nyumba, mifugo mingi tu, maduka, gari, pikipiki n.k) , na watoto wanne wakubwa na mmoja mdogo(9yrs) ila wao hawakujaaliwa watoto pamoja.
Ndani ya hiyo miaka mitatu mama ndio amekuwa akiangalia nyumba, mifugo na shamba lililopo hapo nyumbani.Tatizo limeanza baba alipofariki Cristmass ya mwaka jana.
Siku hiyo hiyo usiku mama akaondolewa chumbani kwake na mumewe, makaratasi ya muhimu muhimu yakakusanywa, kukafungwa na hakuruhusiwa kuingia tena mpaka msiba ulipoisha.Siku ya mali kugawanywa ukatolewa usia hauna tarehe wala sahihi. Mali zote zimegawanywa kwa watoto tu, mpaka mifugo,mama hajapewa hata kijiko.
Familia ya mume ilichofanya ni kumwambia tu anaruhusiwa kuendelea kukaa hapo nyumbani kwao (ila
sio kwake watoto wawili wameshapewa). Kwahiyo ye anaishi tu hajui hatma yake, hata pesa ya matumizi ni mpaka aombe watoto wa mumewe.
Sasa je, kama mke halali wa ndoa, pamoja na kwamba nyingi ya hizo mali alizikuta na mume hakumuweka kwenye wosia hana haki hapo? Hamna ambacho anatakiwa apewe kiwe chake? Akisema apambane na mahakama what are the chances she'll win?