Ndoa na harusi!

nkungwe123

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
444
Reaction score
95
Hbr yenu wana jf
Najua wadada wengi wa Leo mnaishi kimatangazo na hivyo mishebeduo mingiii na sio uhalisia.
Nikirudi kwenye mada, kwanini wadada wengi wa Leo mnashadadia sana harusi zaidi ya ndoa(hata km si zenu)?

kwanini wengi wenu hawapendi kuolewa kwa ndoa tuu bila harusi?(hata km hali inabana).
Heheheheeee..... nawasubiri hapa ili tuliseme hili kwa kina!!
 
harusi inahusika saba jaman hapa tusidanganyane sema ikitokea mfuko hauruhusu hapo sawa itaishia kanisan lakin kama wewe ni mchangiaji mzuri wa matukio ya wenzio kwanin usichangiwe jaman hapo haitaishia kanisan had ukumbin tunaenda mbona
 
Lazma kila mtu aoneee hayawi hayawi sasa yamekuwa
matarumbeta mtaa kwa mtaa
gari ya wazi kila mwenye jicho na ashuhudie hakuna kusimuliwa
 
Lazma kila mtu aoneee hayawi hayawi sasa yamekuwa
matarumbeta mtaa kwa mtaa
gari ya wazi kila mwenye jicho na ashuhudie hakuna kusimuliwa

kumbe,sasa ulivo na foleni si hospital za india zitapata wateja wa ugonjwa wa moyo
 
Harusi ndio zimefanya vijana wengi waogope kuoa, yaani ukizifikiria tu zile gharama basi stimu za ndoa zinakata ghafla kama umeme wa tanesco. Matokeo yake sasa ni kugegedana tuuuuuuu, hatimae kuongezeka kwa single mothers.
Harusi zimewatia vijana umasikini sana. Watu wameuwa hadi mitaji ili waongeze kwenye pesa ya harusi,matokeo yake baada ya harusi kwisha,madeni kibao, na mtaji "kwishnei"
mimi nilishaacha kuchangia harusi ,mana nilijikuta kila mwezi nna kadi hazipungui 10,kila kadi minimum ni 50K, nlijiuliza hivi kwa income gani hasa hadi niwe natoa pesa yote hii?nkaamua LIWALO NA LIWE! Harusi yangu sichangishi mtu hata mmoja. Only waalikwa 50 tu ndio ntakaowaalika na kuwahudumia BURE vinywaji vyakula na mazagazaga yoote yaani NAJIKUNA NNAPOFIKIA TU, sitaki kukwaza watu na michango.
Sijitengi na jamii yangu ila ntachangia NDOA tu za watu wangu wa karibu,misiba,elimu na ugonjwa! Sherehe za harusi,kipaimara,ubatizo,kibaokata,birthday,kitchen party WANISAMEHE TU BUREEE
 
harusi inahusika saba jaman hapa tusidanganyane sema ikitokea mfuko hauruhusu hapo sawa itaishia kanisan lakin kama wewe ni mchangiaji mzuri wa matukio ya wenzio kwanin usichangiwe jaman hapo haitaishia kanisan had ukumbin tunaenda mbona

hapo ndipo tatizo lilipo. kwa nini usigharamie harusi yako mwenyewe, michango ya nini tena?!! wewe andaa kwa kadri ya uwezo wako, hata 4M ni harusi kubwa tu watu watakunywa na kusaza.
 

POLE me ntaazima ata amblanc
 
hapo ndipo tatizo lilipo. kwa nini usigharamie harusi yako mwenyewe, michango ya nini tena?!! wewe andaa kwa kadri ya uwezo wako, hata 4M ni harusi kubwa tu watu watakunywa na kusaza.

lazma uchangiwe wewe ile inaonesha kuna unity,,serikal inachangiwa sembuse ndoa ya tandale kwa mtogole
 
harusi inahusika saba jaman hapa tusidanganyane sema ikitokea mfuko hauruhusu hapo sawa itaishia kanisan lakin kama wewe ni mchangiaji mzuri wa matukio ya wenzio kwanin usichangiwe jaman hapo haitaishia kanisan had ukumbin tunaenda mbona

Waweza changa na usichangiwe.... maana mtindo wa sasa ni chukua chako mapema kisha twende zetu.
 
Lazma kila mtu aoneee hayawi hayawi sasa yamekuwa
matarumbeta mtaa kwa mtaa
gari ya wazi kila mwenye jicho na ashuhudie hakuna kusimuliwa

Mmmh.... dada chumvi hapo ndo nawataka sasa. Wakishaona wadau wa pembeni then maharusi mnabarikiwaje na hilo...?...
 

Big up kaka. A good brother of mine from another mother. Tuko pamoja....
 
mbona hiyo poa sana, hata yangu iko hivyo hivyo sihitaji michango, tena mijitu ya kigamboni wallahi yanasifaaa yakianza kuleta kadi unajikuta mtu wanakuletea kadi ya kitchen party, bag party, send off na harusi yenyewe hapo ni harusi moja tuu package nzima umepewa wewe sasa fikiria familia sita zote zina harusi. kiukweli inabidi tubadilike jamani tufanye kama wakenye wenzetu wanachangia sana elimu na afya badala ya harusi.
 
Kama mfuko wako hauruhusu na huna wa kukuchangia ongea tu na mwenzio atakuelewa.
Kuna pale mkono wako unapofika!!
 
Kama mfuko wako hauruhusu na huna wa kukuchangia ongea tu na mwenzio atakuelewa.
Kuna pale mkono wako unapofika!!

Kuna kesi nimeisikia mdada hataki kuolewa kisa kaambiwa hakuna harusi..... hiki ndio kiini cha post hii. Wadada na harusi kulikoni jamani!!!??? Wakati cku yenyewe mnalia lia tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…