ndoa kamaa hii nan ataikubali?

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,673
wana jamvi wenzangu, kuna jirani yangu hapa anamtafutia mwanae wa kiume mchumba. Kijana mwenyewe ni taahira but kwa tetesi hali hii aliipata ukubwani tena baada ya wazazi wake kutaka utajiri hivyo wakamtoa mtoto awe ndondocha. In real ni matajir sana ila situation iliyopo ni kwamba hakuna mfanyakazi anayetaka kumuhudumia tena huyu kaka ambaye ana miaka 26 sasa. hivyo solution ni kwa yeye kuozeshwa mke tu.

wazazi wamemjengea nyumba kubwa sana na nzuri na pia this week wamemnunulia gari toyota Alexus rangi nyeusi. mama kwa kuwa anazo katangaza dau hapa mtaani kwa binti yeyote atakaye kubali kuolewa naye. swali najiuliza hivi kweli hawa wazazi waliwaza vizuri wakati wanyafanya haya? je sisi wengine tunajifunza nini hapa? utajiri huu wa madudu bora niwe maskini tu.
 
ni wengi mno wamefanya hivi
usione watu na pesa zao, mie hushukuru kwa nilivyo lol
 
ni wengi mno wamefanya hivi
usione watu na pesa zao, mie hushukuru kwa nilivyo lol

Yaani nimeumia sana na nimejiuliza hivi sisi wazazi huwa tunawawazia mema watoto wetu? a tunajali maslahi yetu tu? sasa eti leo kwenye kikao cha kuandaa kitchen party ya mtoto wa jirani ndio anayasema haya. nimejiuliza je anatuwaziaje sisi akina mama tusiokuwa na hela kama yeye? na je huyo binti atakuwa mke au mfanyakazi wa huyo mkaka? jamani tumwogope mungu.
 
Makubwa haya, sasa unaenda kuolewa na taila akikuchinja usiku?
Wanavituo vyao hawa wampeleke huko kama wamechoka kumtunza hawa wazazi,lol!
 
Hao wazazi wa kijana nao ni taahira.

wao ni wazima ila wamemharibu mtoto wao kwa kupenda utajiri jamani lol........ wazazi tumwogope Mungu. sijui hata kabinti katakako hadaiwa kataishije au ndo wanatafuta ndondocha jingine?
 
Makubwa haya, sasa unaenda kuolewa na taila akikuchinja usiku?
Wanavituo vyao hawa wampeleke huko kama wamechoka kumtunza hawa wazazi,lol!

Binafsi sidhani hata kama wamesha jiuliza juu ya usalama wa huyo binti watakaye mpata. Lakini pia kaka mwenyewe ni yule wa kutema udenda tu hajiwez kwa chochote kile. sijui hata huyo mke atamfanyaje
 
haya mambo yapo sana hasa kanda ya ziwa yapo mno.

Kuna baba namfahamu, mwaka 1986 alioa bi mdogo kwa masharti ya mganga kuwa atajifungua mtoto wa kiume taahira.

Mungu si Athuman, yule mama akajifungua binti mzima, huwa namwangalia yule binti ila siwezi mwambia maana hainihusu.
 
dah.....sasa huyo mama atamuhakikishiaje mtoto wa watu atakayeolewa kuwa huyo jamaa hatamdhuru.....?
maana akili ya taahira huenda vile anavyotaka kuipeleka yeye mwenyewe...........
 
Mmh mbona tumeziona ndoa za mataahira, hapa namaanisha sio kichaa, kichaa ndio anaweza kukuchinja kuna wale wenye upungufu kidogo. However, victim wa hizi ndoa ni wale mabinti underpriviledge au wengine huwa matapeli akishapata pesa za kuanzia mtaji anasepa.
 
dah.....sasa huyo mama atamuhakikishiaje mtoto wa watu atakayeolewa kuwa huyo jamaa hatamdhuru.....?
maana akili ya taahira huenda vile anavyotaka kuipeleka yeye mwenyewe...........

Preta hata mimi sijui ila aisee wazazi wa siku hizi hatuwapendi watoto.............. jiulize kweli kijana aliyealiwa mzia kasoma hadi form 3 akaanza utaahira. but maisha yako safi nyumba tu inatisha kiasi kwamba unajiona kama unasindikiza wengine maisha. dunia hii inamambo.
 
Mmh mbona tumeziona ndoa za mataahira, hapa namaanisha sio kichaa, kichaa ndio anaweza kukuchinja kuna wale wenye upungufu kidogo. However, victim wa hizi ndoa ni wale mabinti underpriviledge au wengine huwa matapeli akishapata pesa za kuanzia mtaji anasepa.

wewe umesema kama dada mmoja apa kada angekuwa na uwezo angemtafuta mtoto wa mjini, aingie kingi ili wapate mtaji. ishu ni kwamba kama je na yeye akifanywa taahira? manake kama ni za haya madudu bwana hata kuibika haziibiki
 
haya mambo yapo sana hasa kanda ya ziwa yapo mno.

Kuna baba namfahamu, mwaka 1986 alioa bi mdogo kwa masharti ya mganga kuwa atajifungua mtoto wa kiume taahira.

Mungu si Athuman, yule mama akajifungua binti mzima, huwa namwangalia yule binti ila siwezi mwambia maana hainihusu.

sasa inamaana huyu bi mdogo nayeye alijua kuwa angezaa taahira?
 
Haya mambo ya kuwafanya watoto mataahira yapo sana kwa matajiri..especialy watoto wa kiume! Ni dhambi kubwa mno jamani..sidhani kama kuna mtu atakubali hiyo ndoa ya namna hata kama binti anapenda pesa kiasi gani hapo pagumu sana..
 
madame x mi nimependa tu huo wanja wako kwenye kwenye hii avator yako,vp ulikuwa hiyo lips shine ulikuwa unamechisha na soli ya kiatu ulichovaa? au mkoba?
 
Ni uongo tu, hakuna anayetajirika kwa kumgeuza mtu mwingine taahira; awe mama, baba, binti, mwana, n.k. Kama wametajirika wakati hakuna shughuli ya maana inayoonekana kuwa wanaifanya basi hizo ni hela chafu tu na Bongo hii kitu ni cha kawaida.
  • Ufisadi mkubwa kwenye maofisi ya umma
  • Biashara za madawa ya kulevya
  • Ujambazi
  • Uwakala katika matukio ya kifisadi, kijambazi, n.k. vinavyofanyika nje ya mipaka ya Tanzania
Hizo ndo sababu zinazowafanya watu wawe na utajiri usioelezeka kutokana na shughuli wanazozifanya. Usidanganywe kabisa eti kuna watu wanafanywa ndondocha halafu utajiri ukapatikana. Usidanganyike kabisa!!
 
Back
Top Bottom