omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,444
- 2,700
Habari zenu wanajukwaa.
Kwa wale wanaofuatilia mambo ya Afrika Mashariki na hasa Uganda (kenya wana jukwaa hapa) watakuwa wanajua juu ya hii familia ya Kifalme ya Tooro, Magharibi mwa Uganda ambayo kwa kiasi fulani anaelekea kukumbwa na mabalaa yasiyokuwa rasmi. Ni hii familia ambayo baada ya mfalme kufariki katika mazingira ya kutatanisha na kuacha warithi ambao kimsingi walikuwa wadogo sana, Marehemu Kanali Gaddafi akaamua 'kuwa karibu' na mama yao na kwa upande mmoja akaweza kujenga uwezo (capacity building) ambapo ilifikia sehemu wakaona ufalme unaanza kusimama tena.
Ni mambo mengi lakini suala ninalotaka kuliongelea ni harusi ya kifahari ya binti mfalme. Huyu msichana mdogo baada ya kukatiza mitaa ya ughaibuni akakutana na huyu kijana Christopher Thomas akadhani amefika. Inavyoelekea, Waganda wanaomtakia mema walimshauri huyu dada lakini akawaona hawana la maana zaidi ya wivu na kuamua kuolewa na huyu kijana ambapo nakumbuka baadhi ya habari zilionyesha jinsi ilivyokuwa harusi kubwa na iliyovuta hisia za kitaifa.
Sasa ndoa imevunjika na dada wa watu anairudia jamii ile ile aliyodhani inamuonea wivu huku akijuta na kuacha aibu kubwa kwenye ukoo huo wa kifalme. Kikubwa ni kuwa angalau anajiona 'amepumua'!
Swali langu:
Ukiangalia maelezo ya huyu dada na ukalinganisha muda huu mfupi wa ndoa, je, ni kitu gani huyu dada kafanyiwa!?
(Hakuna tafsiri ya Kiswahili na kama ilivyo kwa Watanzania wengi kutopenda kusoma, hiki kifungu kinaweza labda kuvuta hisia zako)
Soma zaidi hapa
Kwa wale wanaofuatilia mambo ya Afrika Mashariki na hasa Uganda (kenya wana jukwaa hapa) watakuwa wanajua juu ya hii familia ya Kifalme ya Tooro, Magharibi mwa Uganda ambayo kwa kiasi fulani anaelekea kukumbwa na mabalaa yasiyokuwa rasmi. Ni hii familia ambayo baada ya mfalme kufariki katika mazingira ya kutatanisha na kuacha warithi ambao kimsingi walikuwa wadogo sana, Marehemu Kanali Gaddafi akaamua 'kuwa karibu' na mama yao na kwa upande mmoja akaweza kujenga uwezo (capacity building) ambapo ilifikia sehemu wakaona ufalme unaanza kusimama tena. Ni mambo mengi lakini suala ninalotaka kuliongelea ni harusi ya kifahari ya binti mfalme. Huyu msichana mdogo baada ya kukatiza mitaa ya ughaibuni akakutana na huyu kijana Christopher Thomas akadhani amefika. Inavyoelekea, Waganda wanaomtakia mema walimshauri huyu dada lakini akawaona hawana la maana zaidi ya wivu na kuamua kuolewa na huyu kijana ambapo nakumbuka baadhi ya habari zilionyesha jinsi ilivyokuwa harusi kubwa na iliyovuta hisia za kitaifa.
Sasa ndoa imevunjika na dada wa watu anairudia jamii ile ile aliyodhani inamuonea wivu huku akijuta na kuacha aibu kubwa kwenye ukoo huo wa kifalme. Kikubwa ni kuwa angalau anajiona 'amepumua'!
Swali langu:
Ukiangalia maelezo ya huyu dada na ukalinganisha muda huu mfupi wa ndoa, je, ni kitu gani huyu dada kafanyiwa!?
(Hakuna tafsiri ya Kiswahili na kama ilivyo kwa Watanzania wengi kutopenda kusoma, hiki kifungu kinaweza labda kuvuta hisia zako)
...While Thomas has been keen to wash our dirty linen in public, I have remained dignifiedly silent on such supposed private matters.
Soma zaidi hapa