magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Wanajamvi,
Amani kwenu na heri ya mwaka mpya 2016.
Hii ni post yangu ya kwanza hapa kwa mwaka huu wa 2016. Kufanya hivi ni kuthibitisha pia kuwa bado nipo. Matumizi haya ya id fake unaweza kuchukuliwa na muumba na watu wala wasijue.
Ukisoma mada nyingi humu ndani zinazohusu migogoro ya ndoa utasikia watu wakiwashauri hao walengwa wawaone watu fulani kusaidia ushauri wa tatizo lao.
Kati ya mambo ya kipuuzi ambayo wanandoa wengi hufanya ni kupeleka mashitaka yao kwa wazazi,walezi,wachungaji,mapadri,marafiki nk.
Msingi wa ndoa unajengwa na wanandoa wenyewe,mkishakuwa na ndoa inayotegemea akili za wengine hapo hakuna ndoa. Hakuna ugomvi wowote ambao hauwezi kumalizwa na wanandoa wenyewe ni suala tu la kujenga utaratibu wa kuwa na meza ya mazungumzo.
Ikiwa wanandoa wataweka utaratibu wa kutatua shida zao wenyewe hiyo ndoa lazima itasimama. Kupeleka shida zenu kwa watu ni kujidhalilisha kabisa..! Watu wanapenda sifa,wengine wakiwasuluhisha wanasambaza habari zenu.
Me nasema kweli,siwezi kumwambia mtu yeyote mambo ya ugomvi wa familia yangu,naweza kuomba ushauri wa maendeleo,malezi nk. Lkn si ugomvi.
Nawasilisha.