Ndoa anapanga Mungu hali iko hivi kwenye ndoa, Je ingekuwaje tungekuwa tunajipangia wenyewe?

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,515
Nimekaa na kutafakari kwa kina ,nikajikuta najiuliza swali hili,baada ya kungalia changamoto mbali mbali zilizopo kwenye ndoa nyingi ,ambapo wengi tuna amini ndoa huwa inapangwa na mungu,

Nikajikuta Nikajuliza swali, "hivi ingekuweje kama tungekuwa tunajipangia wenyewe?
maana hali hii Mungu anapanga ,Changamoto ni nyingi mpaka unajikuta,Ukiambiwa Swala la kuowa ,Unajikuta kale kaugonjwa kakitoto(Degedege)Kanataka kukujia ukubwani..


Je ingekuwa wanadamu tunajiamulia wenyewe ,Dah sijui ingekuweje,

Nimejikuta tu Nawaza .....

Maana kuna wazee wakorofi sana kwa Hekma zake mungu akawapa wanawake watulivu mpaka raha, ila mzee sasa ndo haeleweki full kunyanya bi mkubwa

Au unakuta kijana kashapoteza Network ya maisha anapata bint mwenye kujielewa na anamrudisha kwenye Mstari,au alikuwa chini basi kwa msaada wa mwanamke anasimama na kuwa juu,

Au upande wapili unakuta jamaa ana haribikiwa kila kitu kisa tu mwanamke,
Au mtoto wa kike anajikuta ana angukiwa kwa mwanaume ambaye haeleweki na kupoteza kila kitu ,mpaka ukimgoogle katika watu walokuwa Duniani humpati ?


Haya yote Ni kwa kuwa mungu anapanga,Tena kwa hekma yake anaejuwa yeye,

je ingekuwa twajipangia wenyewe hali si ingekuwa Tafrani vulu vululu,Shaghala baghala

Nimewaza tu.........
 
Hivi hizi ndoa ambazo zinavunjika baada ya miezi miwili au mitatu zinapangwa na Mungu kweli???? Na kwann apange hivi



Ndoa ambazo deile Ni vita hamna Aman zinapangwa na yeye kweli????
Tunaamini hivyo.
Lakini kama sio hivyo,basi mpango wa Mungu ni mgumu sana kuung'amua na yawezekana kung'amuliwa kwake inahitaji muda mwingi,maombi mengi na kujitoa sana kitu ambacho wengi hatuwezi.Lakini hata wale tilioamini wanaweza wanapata matatizo na kuachana.Sasa mimi nafikiri mpango wa Mungu sometimes ni fumbo.
katika maisha yangu Mpango wa Mungu ni jambo lolote linalonipa furaha na amani na sio uvunjifu wa sheria kwa wakati husika.
 
Hivi hizi ndoa ambazo zinavunjika baada ya miezi miwili au mitatu zinapangwa na Mungu kweli???? Na kwann apange hivi



Ndoa ambazo deile Ni vita hamna Aman zinapangwa na yeye kweli????
mkuu ila si tunaamini ndoa zinapangwa na yeye au maandiko yanasemaje mkuu?
 
Mungu hapangi umuoe nani na ndio maana akatupa utashi.
Mungu aliona kila alichokiumba ni chema ukikitumia vizuri hata mke unapaswa kumchagua ukiwa unatumia vyema utashi wako.
Ndoa ni suala la utamaduni na kila utamaduni una namna yake ya kudeal na haya masuala ya ndoa.
Uwe ulisali sana au hukusali sana ili kupata mke nakuhakikishia changamoto za ndoa zipo palepale.
Tazama ukioa kanisani kwa maombi mengi na mchungaji, shekh au kiongozi wako kuridhia ukipatwa na changamoto utaambiwa hayo ni mjaribu lakini changamoto hizohizo mwingine ataambiwa hayo ni matatizo.
Ndoa ni kupendana na kuendana msipopendana wala kuendana ni matatizo.
Tukizitathmini ndoa kuanzia za viongozi wa dini mpaka waumini ni changamoto tu.
Tazama watoto wa mchungaji wako wanaotokana na ndoa takatifu utaona huruma.
Tuchague wenza kwa akili na utashi alivyotupa Mungu kwani hakutupa akili na utashi bure alitaka tuvifanyie kazi
 
Ukweli ni kuwa wengi hawamuombi Mungu awape wenza mahususi kwa ajili yao.
Wengi wanajichagulia... alaf ndio wanamwambia Mungu.
Ndio maana ndoa nyingi hazidum sababu ya kutokumshirikisha Mungu mwanzoni.
ok ,mkuu naomba nikuulize swali?

je kila kitu ni lazima uwombe mungu ndo akupe?
je mbona kuna maandiko yanasema anaweza kupa pasina kuomba?.
.
 
Tunaamini hivyo.
Lakini kama sio hivyo,basi mpango wa Mungu ni mgumu sana kuung'amua na yawezekana kung'amuliwa kwake inahitaji muda mwingi,maombi mengi na kujitoa sana kitu ambacho wengi hatuwezi.Lakini hata wale tilioamini wanaweza wanapata matatizo na kuachana.Sasa mimi nafikiri mpango wa Mungu sometimes ni fumbo.
katika maisha yangu Mpango wa Mungu ni jambo lolote linalonipa furaha na amani na sio uvunjifu wa sheria kwa wakati husika.
dah ww dada angu umenielewa sana na nahisi darasani ulikuwa wa kwanza

maana najiuliza ndoa nyingi watu wanakesha kuomba lakini bado mungu anawapa mitihani na kuna watu hata kumjua mungu Hawamjui ila wana bahatika kupata utulivu

mungu ni waajabu sana
mkuu sijamchukulia poa na ndomana nimeanisha uwezo wake na hekma yake ,kwa kuwatofautisha watu katika ndoa
 
Unakutana na mwanamke disco then cku chache baadae mmnaoana utasema imepangwa hiyo ? Umetumia uongo kumpata mtu then unasema ndoa imepangwa hiyo ?
kwahiyo mkuu maandiko yanaongopa kwamba ndoa zote zinapangwa pinguni
.ebu nipe ufafanuzi hapo mkuu

nimejikuta nacheka kwa coment yako
 
Back
Top Bottom