Ndiyo tuseme kwamba mapenzi yana wenyewe ama?

Umejipa standards na mwenzako akajipa standards kutakua na mapenzi?

Hii theory yako ni ngumu ikija katika real life.
As you will notice standards ni surefire way of dying alone.

Nilivyo muelewa mtoa mada kazungumza mapenzi anayoyaona ambayo haja experience..
Kama unataka mapenzi ya kweli na wewe uwe tayari kutoa ya kweli..hayaji Kwa yeyote

Ukiwa huna standard kuwa unataka mtu honest
Utachukua Tu yeyote
 
k
kwanini unataka kupendwa??? kwanza tuanzie hapo....
ukishajibu fahamu hili mama na baba yako tayario walishakupenda kwa hiyo hawa wengine unakutana nao kwa sababu tuu ya mtoto, sex basi kwahiyo ukiishi kwa kuamini kutafuta mapenzi ya kweli utaishia kuwa mnyonge kwa muda mrefu ...cha msingi tulia jenga maisha tafuta pesa mapenzi sio sehemu ya kukupotezea muda
 
Unajisikia hivyo kutoka na hali au mfumo wa kimaisha ambao tumeamua kuwa nao miaka hii. Mfumo wenyewe ni matokeo ya umasikini ambao umetoka kwenye hali na kuingia level ya damu. Yaani umasikini wa akili. Haya ndio mambo ambayo mwalimu nyerere alitufundisha kuwa tupige vita umasikini kwasababu madhara yake ni makubwa.

Binti huyu huyu anaekuletea mapozi katika ujana akishakuja kuzeeka huko mbeleni atakuwa tayari kwa lolote. Shida ni kwamba mwili na maumbile yake vinamchanganya akili anahisi kuwa ni mtaji wa kupatia maisha anayotaka kutokana na mitazamo ya tamaa zake za akili za kimasikini.

Imagine binti anawaza kuwa na mwanaume mwenye gari la milioni 30,nyumba ya milioni 100, na kwenye account kuwe na pesa nyingi zisizoisha. Na bado huyu mwanaume awe ni nadhifu na akili nyingi kichwani. Amsaidie yeye na familia na ukoo wake wote.

Hayon yote ni matokeo ya umasikini ambao tunaendekeza. Baba yake asingekubaliwa na mama yake leo yeye angekuwa hapo?!

Kama mama yake alikubali kuanza maisha ya chini na baba yake hadi leo anawakuta hapo yeye anakwama wapi?!

Vibinti vya siku hizi ni sifuri sana linapokuja swala la maisha, vinataka kuwa na maisha ya haraka haraka bila kuyatilia jitihada.

Wao wanaamini kuwa mwanaume ndie anaetakiwa kutoa na kufanya kila jambo kubwa wao ni watumiaji tu. Na hii tunaijenga sisi wenyewe watoto wa kiume na jamii kwa ujumla.

Tunawaendekeza na ndio maana wao wanaichukulia ni sheria kwa maana jambo la mazoea huonekana ni la kawaida, na kawaida ni kama sheria.

So wewe usihangaike nao hao. Timiza malengo yako ya msingi sababu hata ukiwa nao still watakupa tu presha ya kuyafikia malengo hayo hayo.
So be your own agenda, be your own man, be your own caretaker, be your own final decision maker. After some time utaona kawaida sababu wewe unapambana na nature ila wao wanapambana na mambo na fikra za mpito.

Iliandikwa wapi kuwa mwanamke ataiacha familia yake na kwenda kwa mwanaume mwenye Crown athlete, nyumba nzuri na kazi ya mshahara wa milion 3. But iliandikwa kuwa mwanamke na mwanaume wataacha familia zao na kujiunga pamoja kupambana na maisha.

Mwanamke ambae anakataa mwanaume ambaye ni mpambanaji sababu hajapata huyo sio mwanamke ni msichana na hajui maisha ni kitu gani. Na ukiona umeanza kufanikiwa tu kuwa makini sana na namna unachagua wanawake hawa wa kizazi hiki. Ni mara mbili upige punyeto kuliko kuweka ndani hawa viumbe kipindi hiki cha kuhangaika na maisha magumu.
 
Wadada wana taka 'mahensamu', pesa iwepo, bado uwe na kifua kipana, uwe mrefu, uwe na sauti nzito, uwe na nyumba na kausafiri, rangi yako iwe nzuri, uwe romantiki, yaani in short mambo ni mengi sana...
 
Wadada wana taka 'mahensamu', pesa iwepo, bado uwe na kifua kipana, uwe mrefu, uwe na sauti nzito, uwe na nyumba na kausafiri, rangi yako iwe nzuri, uwe romantiki, yaani in short mambo ni mengi sana...
Wakaka pia wanataka wenye ma wowowo miguu minene mambo ni mengi pia hata kwa wakaka
 
Sema cha kusikitisha ni kwamba watu wengi wanachanganya kati ya "kujipenda" na "kuringa" mtu ukijipenda unaambiwa unaringa
 
Umemaliza kila kitu pumzika mkuu
 
mwanaume ukiwa unalialia kuhusu "mapenzi" daah,

Nakuona mtu wa ajabu sana

emotion decision for true man only
 
sanaaa na ume eleweka vilivyo.
 
@The Boss as your name
 
Mkuu gwankaja kwanza nikupe pole kwa unayoyapitia but personally sikumbuki kukaa nikawaza kumpenda sana mwanamke sasa sijui ni uelewa wangu mdogo au nini!!!mke wangu ninayeishi naye mwaka wa nane huu kuna wakati kipindi hiko kabla hatujaowana alivunja mahusiano kwa takribani (sina kumbukumbu nzuri) ila ni kama miezi 2/3,yalikuwa maneno machache tu aliandika kitu kama “nimekuchoka na tabia zako niache na maisha yangu”,hii text niliipata nikiwa nimekaa na jamaa zangu so niliifungua sms nikasoma nika-lock simu nikaweka mfukoni nikaendelea na mambo yangu,hapo tuna mahusiano ya miaka 6 nyuma coz tumeanza mapenzi yupo aged 15 akiwa form II mimi 18.

Jioni nikampigia simu maana sikuelewa sababu ya kauli ile ili nijue ila hakupokea,nikafuta namba na sikumtafuta tena kilichokuwa kinaisumbua akili ni namna gani nitampata mwanamke nitakaeweza kumtengeneza aendane na ninavyotaka mimi (though tabia zake zilikuwa nzuri kiasi na nilimkuta mtoto bado) ila kama siku mbili mbele nikasahau,alikuja kurudi mwenyewe akinituhumu roho mbaya kubembeleza sijui nikamwambia tu live kwamba mimi nataka tufanye maisha huo muda wa kuanza kutumiana jumbe kwamba hivi na hivi sina,kweli nilipojiona umri unaruhusu bila kujali ni mrembo au siyo mrembo,ana elimu au hana elimu nikaona huyu huyu nitatembea naye nikiwa na sababu zangu hasa utii aliokuwa nao kwangu na kwa ndugu zangu,sijawahi kuwaza nampenda ila kumthamini na kumuheshimu as long as akizungua naondoka na heshima zangu kwake,sina hasara.

Why nimeandika haya yote?kama lengo ni kutafuta mwanamke wa kukustarehesha nje ya maisha yako seriously,mtengeneze kichwani mwako,muumbe utakavyomuumba kwenye ubongo wako,weka shape sijui miguu ya bia jicho kokoto kisha wewe ingia mtaani utakutana nao chungu mbovu,ila kama unategemea uje ufanye naye maisha aendeleze uzao wako chagua tabia mzee huyu huwezi kumuumba kwenye ubongo wako,kingine usiishi na mwanamke huku ukijua unampenda sana kama wanavyolia lia vijana miaka hii,itokee tu unfortunately umejikuta ktk hali hiyo ila epuka hiko kitu maana akijua udhaifu wako kwake utachizika,nimeshuhudia,nasisitiza akili zitakuruka hawa viumbe version yao haipokei tena updates akikubadilikia utalitamani kaburi.

Mwanamke mthamini/mjali na muheshimu kwa dhamana anayokushikia kukuzalia watoto,sometimes kuwatunza etc hii sifa hata ukimpa atafarijika japo ni jukumu lake ila ukijifanya kumpenda sana hautakuwa na maisha sawa sawa duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…