Erick MR
Member
- Nov 11, 2022
- 77
- 152
Jana nilikua namsikiliza dada mmoja maarufu kwenye kipindi kimoja akielezea mkasa uliomkuta baada ya kumsaidia mpenzi wake ambaye alikua hana kazi wala pakukaa, kwakua yule dada alikua ameajiriwa na anapokea mshahara mzuri akamchukua akawa anashi naye kwake na kumhudumia kwa Kila kitu hadi shopping (nacheka kama mazuri).
Ikapita miezi siku bwana yule akamfuata mpenzi wake ambaye ni huyo dada akamwambia anashida anomba amsaidie kiasi cha Pesa kama milioni hivi Ili atatue hiyo shida kisha angemrudishia kiasi kile lakini yule dada akamwambia kwamba bado mshahara haujaingia hivyo asingeweza kuwa na kiasi hicho kwa muda ule.
Mapenzi yana nguvu bhana jamaa akambembeleza yule dada akope kisha ampatie atatue shida yake kisha mshahara ukiingia atalipa alipo kopa yule mdada akakopa Kweli akampatia jamaa lakini cha ajabu siku zikawa zinaenda jamaa harejeshi akawa anampiga kiswahili tu na yule mdada anasumbuliwa na kampuni ya mkopo (kausha damu ) kwenye riba.
Baada ya muda kupita ikatokea bahati kwa yule jamaa akapata kazi serekalini yule mdada akajua labda ndo ingekua mwisho wa matatizo lakini chajabu zaidi mchizi hakulipa lile deni akawa anafanya matanuzi na Pesa zake Kuna kipindi simu zikawa haziiti kabisa.
Masikini yule dada baada ya riba kuwa kubwa na kampuni kumtisha tisha kwamba watapiga mnada vitu vyake kwa kwepa aibu kwasababu yeye ni maarufu aliamua kuuza Kila kitu chake cha ndani alichoanza nacho maisha nakulipa lile deni.
Je wewe mwana jamii mwenzangu ni kipi umeshawahi kufanya cha ajabu kwajili ya mapenzi na huwezi kukisahau kabisa?