Ndio mwisho au naomba ushauri

chavka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
223
Reaction score
46
Nimamkini muwazima wanajamii. Kwangu salama kiafya. Naombeni ushauri juu ya hili
Nina miaka 3 ktk ndoa yangu lkn toka nilipoacha kazi na kujiunga na chuo maisha ya ndoa yamekuwa magumu tena ukuchangia ninaishi na mama mzazi pamoja na mdogo wangu wa kiume kipato anasoma darasa la 6 mwakani 7 na mtoto wa mama mdogo wangu anasoma la 3. Sasa mwenzangu simwelewi mara kununa mara anatoa maneno yasio na msingi na yote yametokana na mm kwenda kumtembelea Dada yangu nikachelewa kurudi kafika maala anamwambia mama yake kuwa wanaume wako wengi anaeza kupendwa na hata wanaume wengine, kuolewa si lazma. Kiukweli ni mtu wa kupayuka hajui kuzungumza kama mume na mke. Sijui kunanini nimezaa nae mtoto 1 na anaishi na shangazi yake hapa kwangu sina dada wa kukaanae kulingana na majukumu. Sielewi huu ndio mwisho wetu au nifanyeje maana kwa upeo wangu nashindwa kuvumilia
 
Pole huuu sio mwisho
huu ni mwanzo wa maisha ya ndoa lol
 
mmmh mtoto wenu yupo kwa shangazi but wa ma mdogo wa darasa la tatu mko nae?something is wrong some where
 
Ahsante boss. Kivipi purple? Mtt kuwa kwa shangazi ni kutokana msaidizi wa ndani hayupo mm natoka asubuh na mwenzangu hotoka asubuh kurudi usiku. W'end ndio tupo home. Huyu wa darasa la tatu anajitambua na anauwezo wa kujiwekea chai na kufua ndio maaana nipo nae. Ile The Boss leo kamtolea maneno makali sana huyu mtoto alikuwa anafuta meza ya chakula akamwambia msininyanyase naweza kuliacha jumba lenu tena akamkanya kwakitendo cha kuosha meza sikusema kitu nimekaa kimya mpaka now sijui nifanyaje
 
Last edited by a moderator:
Mi nakwambia ukweli tu HAUPO SENSITIVE NA MASUALA YENU YA KIPESAAA!!!!!!!!!! Habari ndo hiiii! Mwenzio anakereka maisha magumu wewe

1. Kazi umeacha ukaanza chuo!
2.Kana kwamba haitoshi unajaza nduguzo hapo kwenu bila kujali kama mwenzio anajisikiaje juu ya hilo zigo la watu ulilomjazia!
3. Hauko sensitive kumjali mwanenu wa kumzaa ila nduguzo unawajali kweli kweli! Hiyo hela ya kulisha watu wote hao si ingekutosha kumlipa msichana wa kazi na kujiendeleza!
4. Unatafuta tatizo wakati tatizo unalijua ni weweeeeee na nduguzo! Hata kama ni mie japo nakupenda huwezi kunilazimisha niwapende na nduguzo kama wewe! Wangu mwenyewe nimewatelekeza!
5. Nduguzo wasaidie ila huko huko waliko! Kama shule ziko kila mahal!

Mi nakupa kitchen party ya bureeeeee! Utaivunja ndoa yako afu ndugu zako watakuchekaaaa! Sadiia ndio ila waliko! Warudishe wote kwao, mrudishe mtoto, leta hausigel muombe mumeo msamaha na umwambie umejua makosa yako! Nxt time kabla hujaamua jambo angalia na hisia za mwenzio juu ya hilo jambo!

Kila mwanaume akitoka kazini anataka makute mkewe na watoto wanamngoja kwa furaha na upendo si umati wa mtume, na kesi zisizoisha na vizinga kila kukicha! Nyumba inakuwa chungu! Hayakuwa makubaliano wakati mnaooana!!!!!!

Ukiendekeza ndugu, hutojenga! Hutonunua gari, hutoishi maisha ya raha na kuenjoy! Saidia inapobidi ilia huwezi kumaliza matatizo yao! Jifikirie wewe, mwanao na mumeo! Nimekwambia Kiroho safiii!!!!!!!!!
 
nakushangaa sana.....kilichokufanya uache kazi ni nini kama huna plan B ya kipato? Ina maana mjeo pekee ndo anasukuma gurudumu? umezungumza nae kuona kama anamudu bila shida kutunza ukoo huo?

wenziohuwa hawaachi kazi mjomba..... Akiacha lazima uwe na biashara ya kukuingizia angalau faida ya 10,000 kwa siku....... Hujui mwanume majukumu?

Anyway zungumza na mkeo
 

Nashukuru kwa ushauri wako japo mm ni mwanaume na ninatatizo na mke wangu. Ila kuhusu mtoto nikwamba msichana alikuwepo akaondoka pindi mama yake alipokuwa anaumwa na toka hapo sikupata msichana wa kazi mpaka sasa. Na kuhusu ndugu sio kama nimewakumbatia kwa kiwango hicho bali ni kawaida. Nampenda mwanangu na ndio maana pia nasoma kwaajili yake nimwandalie maisha yaliobora kuliko nilioishi mm mwangu nikila kitu kwangu ndio ananifanya niishi na kuyatafuta maisha kwa nguvu zote.
 
Ndoa ni sawa na zigo la misumari kulibeba lazima uwe na akili kama kichaa
 

Usemacho ni sahihi kuwa mwanume majukumu ila kiukweli naitunza familia yangu pasi na kumtegemea yy hata kidogo na sijawahi kumuuliza juu ya pato lake. Namshukuru mungu Rizki ya kujitosheleza bado ninayo na nina akiba ya kujitosheleza mpaka namaliza kusoma niliacha nikiwa nisha jiwekeza vya kujitosheleza. najua gharama za kusoma nimejipanga ndugu
 

Sorry kwa kuchanganya madesa! Ila sie wanawake haswaa wa mjini hatupendi ndugu! Ndugu zako wakarimu kwako ila usihadaike itakuwa wanampasua kichwa wife!!!!!!

Usipojiangalia ndoa kwishney! Wasaidie waliko! Mi nakwambia from Experiance! Wewe unaweza kutoelewa kwanini mkeo haoni vitu in ya point of view ila its frustrating!

Numbani kama kituo cha polisi! Kuku mmoja hatoshi!!!!!! Ndugu anauma ila kwa wewe ndugu yake ila kwa mwenzio mzigo! Sasa maadam na wewe umekuwa tegemezi its better ukaelewa the odds na kusawazisha! Damu nzito watakusamehe tu nduguzo!!!!
 
Mwanangu Chavka huna haja ya kufikia hitimisho. Ndoa ndoana na hakuna ndoa isiyo na vijimambo. Muhimu badala ya kuhukumu kwa hisia kaa na mwenzio umuulize sababu ya hayo masahibu anayosababisha. Jaribu kumsikiliza kwa makini na ukishajua msimamo wake toa mapendekezo na msimamo wako ukilenga kujenga na si kubomoa. Pia ufanye timming ya kuongea naye.Siyo aanze kurusha mibomu yake nawe uanza kujibu kwa mibomu yako.Namna hii mtabomoa. Mwambie kuwa hao wanaume anaodai wapo ni kama wewe. Wanayo matatizo yao maana nao ni wanadamu na si malaika. Anaweza kumkimbia mjusi akajikuta ameingia kwenye mikono ya mamba. Utulivu wa ndoa ni matokeo ya juhudi za wanandoa kujuana misimamo, mipango, tabia na matarajio. Kwa leo naona niishie hapa. Muhimu unapaswa kufanya utafiti na uchunguzi kujua chanzo ni nini na nini welewa wa mwenzio. Jua upande wake na ujaribu kuvaa viatu vyake kama ambavyo umwambie avae viatu vyako then atoe jibu.
 
LARA usijali kwa mwanadamu kukosea ni kawaida.
Nimekuelewa kwa undani sana na umenikumbusha kitu now daahh kumbe nilikuwa sijui kama changu takataka chake Dhahabu maana anamdogo wake wa mwisho nilichukua dhamana ya kumsomesha na kamaliza mwaka huu na hapa nilikuwa na mpango wa kumtafutia pakujishikiza lkn kwa mtaji huu napiga atua mbili nyuma sio ndugu zangu tu hata mwanangu wanaweza kuja kumnyanyasa kama mpango ndio ulivyo
 
Last edited by a moderator:

Kutokana na maelezo yako ya mwanzo wewe ni mwanaume?, ndio ulieacha kazi ukaanza chuo?, ndio mara ukienda kwa dada yako unamkuta amenuna?, mbona maelezo yako yapo kike kike, maajabu.
 
mjuni nadhani hauja elewa vyema kwan mm siwezi kuwa na dada?? Kwetu tumezaliwa 6 mi wa tatu na wapili kuzaliwa ni dada yangu. So nimesema nikipia au kwenda kwa dada na maana kumtembelea yy hununa lkn huyohuyo dada ndio anaishi na mwanangu
 
Last edited by a moderator:

Ahsante kwa ushauri wako namuomba mola anipe hekma juu ya haya
 
Swali tu la kiugomvi, mamako mzazi nae anafanya kazi? Manake mna mtoto msieweza kumlea ila mmejaza nyumba full. Pole mwayego, naona The Boss keshakujibu.
 
Last edited by a moderator:
Swali tu la kiugomvi, mamako mzazi nae anafanya kazi? Manake mna mtoto msieweza kumlea ila mmejaza nyumba full. Pole mwayego, naona The Boss keshakujibu.

Ahsante,Kiujumla mama ni mzee hafanyikazi na huduma sio tatizo maana kila akitakacho apata. Na mtoto sio kama hatuwezi kulea ni kukosa msaidizi mama kwa umri wake hawezi tena ulezi analea kibibi
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…