Ngurubhe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,840
- 1,048
Jiwe analotupa huyu jamaa linaweza kumpiga mtoto au adui yake..ndicho tunachofanya Tanzania.Tunatupa mawe lkn hatuelewi yanaelekea wapi!.
Habari!.
Unajua nimekuwa najiuliza sana kwa Tanzania tunamikataba mingine tunawapa migodi kwa miaka 100;wazungu wanachukua mchanga wanaenda nao kwao,mara EPA,RICHMOND,ESCROW na mengine kibao kumbe wanaohusika wanakuwa wanajua kusoma tu.
Unajua hata kasuku anajua kusoma,roboti pia?.Lakini havina uwezo wa kutafakari na kuchambua juu ya kilichosomwa.
Leo hii serkali bila uoga,bila aibu,bila hata simile huku wakitabasamu wanasema eti sio lazima viongozi waandamizi wa vitengo nyeti wae na elimu nzuri ati na. Vyeti sahihi...sio lazima.
Hii itakuwa ni Tanzania tu.so primitive we are....haipo kwingine Duniani..
Inawezekana rais umeona uweke hivyo ili ukiongea wasiwe wanatoa resistance,lakini yote haya yanatupeleka wapi kama taifa?.
Taifa linaloongozwa na watu wanaojua kusoma tu,na wanaofoji ni sawa na dereva kipofu anaejua kuongea tu na lesseni aliipata mtaani.