NDEJEMBI: Wanafunzi Msiwatege Kingono Wahadhiri wenu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi amewataka wanafunzi kutowatega wahadhiri wao kingono ili kuwaepusha kuingia katika vitendo hivyo. Ndejembi alisema hayo jana, wakati akifungua kongamano la kukuza maadili na mapambano dhidi ya rushwa lililoshirikisha Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Alisema rushwa ya ngono ni miongoni mwa changamoto zinazovikumba vyuo mbalimbali duniani.

“Madhara ya rushwa ya ngono ni wanafunzi wasiostahili wanaweza kupewa alama nyingi kuliko wanazostahili, hii inaweza kumhusu mwalimu wa kiume akishirikiana na wanafunzi wa kike,” alisema Ndejembi.

Pia, alisema wahadhiri wa kike wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kiume na kwamba hasara ni kuzaliwa kwa wasomi ambao hawana tija na kuwanyima haki wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao.

“Jambo hili ni sumu kwa maendeleo ya taaluma na nchi kwa jumla. Ni wajibu kwa kila mtu anayependa maendeleo ya nchi hii kukemea kwa juhudi zote,” alisema Ndejembi.

Aliwataka wanafunzi kuendelea kutoa taarifa za wanaojihusisha na vitendo hivyo bila kuwasingizia, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa sababu Serikali inataka kutokomeza rushwa hiyo katika taasisi za elimu ya juu.

“Lakini tunasikia wanafunzi wenyewe mnawatega wahadhiri wenu, baadaye mnakuja kusema kuwa hapana ameniomba rushwa ya ngono,” alisema Ndejembi.

Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Lughano Kusiluka aliwapongeza wanafunzi kutokana na kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kwao.

Alisema Serikali ya chuo inaonyesha jinsi gani inafanya kazi vizuri, ndiyo maana wanafunzi wamekuwa wengi katika kongamano hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni mazingira gani yataonyesha mhadhiri kategwa, maana mademu tayari ni nyavu zipo kila mahali.......sasa mhadhiri ataamua akanase kwenye nyavu zipi na asinaswe na nyavu zipi. Kwa hiyo utaona tatizo hapa siyo nyavu, ni yule anayeziingia nyavu ili zimnase.​
 
Sasa hivi wamegeukia kwa wanaume waenzao, wahadhiri wa kiume wana waharibu sana wanafunzi wa kiume, wana warubuni kuputia marks na kuwaharibia mfumo mzima wa masomo.

Uwiiiiiiii Jah anusuru kwa kweli.
 
Sasa hivi wamegeukia kwa wanaume waenzao, wahadhiri wa kiume wana waharibu sana wanafunzi wa kiume, wana warubuni kuputia marks na kuwaharibia mfumo mzima wa masomo.

Uwiiiiiiii Jah anusuru kwa kweli.
Ulianza 'kuharibiwa' chuoni?
 
rushwa ya ngono vyuo vikuu ni jambo la kwaida sana.
ngono inanuka balaaa.
wapo wahadhiri wachache wanao jiheshimu, lakini pia wapo wanafunzi wa kike wachache wanao jiheshimu.
 
Huu ushauri wa kipumbavu... mwenye dhamana ni mwalimu, hapaswi kufanya mahusiano yasiyofaa na mwanafunzi, no matter what. Mwalimu ndio yupo kwenye position of authority, ni jukumu lake kujiheshimu.
 
Huyu so called waziri akwende huko na mfumo wake dume! Hao walimu ni wanyama wasioweza kuamua? Na hao wa kiume wanaolawitiwa anasemaje? Ongea na hao wahadhiri, ndo janga la kitaifa!
 
Back
Top Bottom