"JAMBO LA MAMA LIMETIMIA-NDEJEMBI"
Anaandika Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Deo Ndejembi
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa 23.3%.
Mhe Rais ameonyesha wazi kwamba ameweka maslahi ya watumishi wa umma mbele. Sisi wasaidizi wake tutahakikisha maagizo yake na maono alionayo juu ya kuboresha utumishi wa umma yanatekelezwa kwa wakati.
Toka aingie madarakani amepandisha madaraja watumishi zaidi ya 200,000. Amelipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi 104,350 yenye thamani ya billioni 154.5. Amepunguza makato ya kodi ya mshahara (PAYE) kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8 ambayo pia ina effect kwenye mshahara. Mhe Rais alifuta retention fee kwa wanufaika wa bodi ya mikopo. Na kwa budget ya mwaka 21/22 Mhe Rais ameridhia kupandisha madaraja watumishi 91,000 ambao utekelezaji umeanza mwezi huu.
Mhe Rais kaonyesha imani kwa watumishi wa umma. Imani hii ni deni. Tumlipe kwa kufanya kazi