Ndege yaanguka na wanajeshi 92 nchini Urusi

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
_93122299_russiawarplane.png


Image copyright AFP
Image caption Ndege ya kijeshi ya Urusi imeanguka huko Black Sea
Kuna hofu kuwa huenda abiria wote 92 wamefariki baada ya ndege ya jeshi la Urusi waliokuwa wakisafiria kuanguka baharini katika eneo la Black Sea.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema kuwa imepata mabaki ya ndege hiyo baharibi kilomita moja unusu kutoka Sochi.

Ndege hiyo muundo wa Tupolev-154, ilikuwa na abiria 91, wakiwemo wanajeshi wa Urusi na kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble.

Walikuwa wanatazamiwa kupiga mziki wa bendi ya mkesha wa mwaka mpya katika kambi ya jeshi la wanahewa karibu na mpaka na Syria huko mjini Latakia.
_93122301_alexandrov.jpg


Image copyright AFP
Image caption kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble
Ndege hiyi ilipotea katika mitambo ya Rada, muda mfupi baada ya kupaa angani, kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya Black Sea huko Sochi.

Ndege yaanguka na wanajeshi 92 nchini Urusi - BBC Swahili

Ndege ilioanguka: Rais Putin ataka uchunguzi Ufanywe

_93123657_putin.jpg


Rais Putin ameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu ndege ya jeshi la Urusi, iliyoanguka katika Bahari ya Black Sea, punde baada ya kuondoka Sochi, ikielekea Syria.

Hakuna aliyenusurika kati ya watu zaidi ya 90 iliyobeba.

Televisheni ya Urusi imecheza rekodi ya mawasiliano ya mwisho baina ya wanaoongoza safari za ndege ardhini na rubani wa ndege hiyo.

Hapakuwa na ishara ya matatizo, na rubani alisikika ametulia, hadi ndege ilipotoweka.

Abiria wengi walikuwa kutoka kikundi cha bendi ya muziki cha jeshi kikundi cha Alexandrov Ensemble kilichopata sifa.

Ndege ilioanguka: Rais Putin ataka uchunguzi Ufanywe - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom