Ndege ya India yakatiza safari sababu ya panya

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,856
Ndege iliyokuwa safarini kutoka Mumbai kwenda London ililazimika kukatiza safari na kurejea uwanja wa ndege baada ya panya kuonekana ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo nambari AI 131 ilikuwa imefika Iran pale panya alipoonekana na mmoja wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ripoti zinasema.
Abiria waliendelea na safari yao kwa kutumia ndege nyingine.
Shirika la Air India limesema ndege hiyo itanyunyiziwa dawa ya kuua wadudu na kwamba uchunguzi unafanywa kuhusu madai hayo ya kupatikana kwa panya huyo.
Shirika hilo limesema wahandisi wa ndege wanaendelea na uchunguzi “ingawa haijathibitishwa iwapo ni kweli kulikuwa na panya.”
Maafisa wa shirika hilo wamesisitiza kwamba uamuzi wa kukatiza safari ulichukuliwa kwa maslahi ya usalama wa abiria.
Panya wanaweza kuwa hatari wakiwa ndani ya ndege kwani wanaweza kutafuna nyaya.
BBC
 
Hahahaaaaaa, kobongo bongo hilo jambo haliwezekani, hata wakiona nyoka,

Labda awe anaconda
 
Ndege iliyokuwa safarini kutoka Mumbai kwenda London ililazimika kukatiza safari na kurejea uwanja wa ndege baada ya panya kuonekana ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo nambari AI 131 ilikuwa imefika Iran pale panya alipoonekana na mmoja wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ripoti zinasema.
Abiria waliendelea na safari yao kwa kutumia ndege nyingine.
Shirika la Air India limesema ndege hiyo itanyunyiziwa dawa ya kuua wadudu na kwamba uchunguzi unafanywa kuhusu madai hayo ya kupatikana kwa panya huyo.
Shirika hilo limesema wahandisi wa ndege wanaendelea na uchunguzi “ingawa haijathibitishwa iwapo ni kweli kulikuwa na panya.”
Maafisa wa shirika hilo wamesisitiza kwamba uamuzi wa kukatiza safari ulichukuliwa kwa maslahi ya usalama wa abiria.
Panya wanaweza kuwa hatari wakiwa ndani ya ndege kwani wanaweza kutafuna nyaya.
BBC
ingekua bongo mbona poa tu sema wazungu waoga sana
 
Niliona hii taarifa jana Aljazeera nikacheka sana sana. Eti Pilot karejesha ndege kisa panya! Je ingekua ile inayokwenda Mikoani kila siku ambayo ina kila mdudu humo ndani ingekuaje?
 
kibongobongo hapo ni mwendo mdundo panya ni sehemu ya maisha yetu labda angekuwa simba tungemfikilia
 
Back
Top Bottom