Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Ndege hiyo yenye teknolojia ya kisasa imetengenezwa kwa miaka 10 na kuvumbua teknolojia 102 mpya. Hivi sasa makampuni 23 za aina ya ndani na nje yameagiza ndege 570 za aina hiyo, ikiwemo kampuni ya huduma ya anga ya Marekani (GECAS).
Ndege hiyo iliyopewa jina la C919 imeundwa kutoa ushindani kwa ndege aina ya 737 Boeing ya Marekani na A320 Airbus kutoka mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Ujerumani.
Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikaa angani kwa dakika 90 kisha kurejea salama katika uwanja wa Pudong, mjini Shanghai.
Ndege hiyo ilifika kasi ya kilomita 300 kwa saa (maili 186) licha ya kuwa ndege hiyo imetumia teknolojia kutoka nje ya nchi hiyo, kwani injini zake zilitoka kampuni ya CFM International yenye viwanda Marekani na Ufaransa. Katika safari hiyo, ndege hiyo iliwabeba watu wachache sana, marubani watano pamoja na wahandisi.
Shirika linalosimamia usalama wa safari za ndege Ulaya limeanza utaratibu wa kutathmini na kuidhinisha ndege hiyo ya C919 ambayo ni hatua muhimu kwa ndege hiyo ndipo iweze kufanikiwa katika soko la Kimataifa.