Ndege iliyowabeba watu 21 yatoweka Nepal

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Ndege ndogo iliyowabeba abiria 21 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.

Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo imeanguka.

Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Tara Airlines.


Chanzo: BBC

==============

UPDATE

Abiria wote 23 waliokuwepo kwenye ndege ya kampuni ya Tara Air iliyoanguka mapema leo Magharibi mwa Nepal wamekufa, mamlaka zathibitisha.
 
Duh aisee pole zao sana, MUNGU awapiganie, ni miongoni mwa usafiri ambao siupendi kwa ukweli, si upendi basi tu
 
Ndege ndio usafiri salama 99% ila sema hizo ndege ni za muda mrefu sana.
 
Back
Top Bottom