iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,927
Ninaamini hiki ni kipindi cha mavuno kwa mawakili ambao watakuwa wakifanya Kazi ya kuinyoosha serikali mahakamani ili ifuate utawala wa sheria.
Kesi mamia kama si maelfu zitafunguliwa na wananchi na makampuni kudai fidia za kudhalilishwa au kunyanganywa mali zao.
Suala la majipu ni mojawapo,suala la kunyanganya watu mashamba,suala la kupokonya sukari,kufukuza watu bila kuwasikiliza,serikali kugoma kulipa baadhi ya madeni halali na mengine mengi.
Naamini waziri wa sheria ni mbobezi lazima ameshamwambia kwamba haya mambo yataitia hasara serikali kwa matrilioni,na kama vile somo halijaeleweka naona mchezo wa kucheza na haki za watu unaendelea kwa hoja mfu kwamba hao watu walikosea kwanza hivyo hawapaswi kupewa haki!!
Nataraji ndani ya Mwaka huu na ujao mahakama kujaa utitiri wa kesi za madai ya matrilioni na ambazo kwa asilimia mia serikali itashindwa,tusiwalaumu mawakili wa serikali pale serikali inaposhindwa kesi,mpaka kesi imfikie wakili wa serikali,tayari mambo yameshaharibika,kwa mfano tamko la kufukuza mtu jukwaani Iinatolewa papo hapo bila kumshirikisha halafu serikali ikishtakiwa unataraji ishinde!!!
Viongozi wanaogopa kushauri wameacha jahazi lizame ili iwe sehemu ya somo,Sokoine alitawala kwa kipindi chake ambacho hakilingani na hiki,sasa wananchi wana uelewa na Uhuru mkubwa wa kudai haki,watazidai na nafikiri serikali imeliona hilo.
Tuliwahi kubomoa sheli ya mMansoor pale Mwanza tukalipa mabilioni,bado mabilioni ya kesi ya Samaki wa Magufuli,hizo ni baadhi tu ya kesi zinazoweza kuwa somo Zuri kwa serikali na wananchi kwamba fidia hizo ni kodi zetu,kama maamuzi mazuri yangefanyika kwa kufata sheria tungezitumia kujenga barabara,zahanati,madawati,shule.