Kuna mama mmoja alikuwa anatokea posta kuelekea ubungo,mtoto wake mchanga alikuwa analia sana,yule mama akamtolea ziwa mtoto anyonye lakini mtoto hakutaka kunyonya. Yule mama akamwambia mtoto-"usiponyonya nampa huyu baba maziwa anyonye"(baba aliyekuwa amekaa jirani na yule mama). Bado mtoto aliendelea kulia tu bila kunyonya. Yule mama akaendelea kusema-"utanyonya au nimpe huyu baba anyonye". Yule baba akadakia na kusema -"wewe mama mbona haueleweki,unanipa ninyonye au hunipi?maana mimi nimeshapitiliza vtuo viwili nasubiri uamuzi wako"¤