Ulimakafu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 31,806
- 13,763
Kwenye daladala lifanyalo safari zake kati ya Kariakoo na Mbagala kulitokea wizi wa pochi ya mtu mmoja wa makamo,akiwa hajui hili wala lile wakati wa kutaka kutoa nauli walipofika Mivinjeni, kutanabahi hamna pochi mfukoni.Kwa mkwara mzito akatangaza aliyemuibia amrudishie haraka la sivyo atakiona cha moto,lakini hakuna hata aliyeshtuka wala kujali.Akatangaza tena huku akianza kuvua viatu,soksi,kukunja suruali,shati sambamba na kuvua barakashia na kuiweka mfukoni.Akarudia tena kutangaza sasa akianza kujiapiza kuwa aliyeiba atakiona cha mtema kuni kama haijarudi afikapo Mtoni kwa Aziz Ally,kama alivyofanya juzi.Kuona hivyo pochi ikarushwa toka nyuma ya daladala kwenda kwa yule mzee,ikawa kimyaaa.Abiria wengine wakamuuzia yule mzee ulikuwa unataka kumfanya nini mwizi wako?Akajibu:Nilikuwa najiandaa kutembea kwa mguu kwenda Mbagala.