NDANDA kuchele! Hiyo ndiyo habari ya mjini baada ya timu hiyo ya Mtwara kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara, ikiwa ni mara yao ya kwanza tu kucheza ligi hiyo.
Ndanda iliifunga Stand United mabao 4-1 na kuwa timu iliyopata ushindi mkubwa zaidi kwenye mechi za kwanza za ligi.
Yanga iko katika nafasi ya 13 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 14 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar wakati Simba ikiwa katika nafasi ya saba baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Coastal Union.
Ni mambo ambayo hayakutarajiwa lakini yameshatokea. Haya yamejitokeza wikiendi iliyopita.
MwanaSPoti